Nissan Dualis: Dxf Nyingine Imewaka Moto

Poleni. Ila kwa nini uweke vifaa zaidi ya vilivyopo ktk gari? Na kama ni lazima, ni vizuri kutumia mafundi wenye uzoefu au dealer wa aina ya gari husika.
 
nilishawahi jiuliza sana zile rubber huwa zina msaada gani?😂😂kumbe ni urembo tu!!!! Basi nilikiwa najua pengine milango inalegea hivyo wanakazia hiyo midude
Na kuna raba fulani wanaweka kwenye milango, ha ha mi hizo mambo ndio mbali mbali kabisa.
 
Nna jamaa yangu mmoja kafunga hizo makitu kwenye jeep yake aliyoifanyia modification.[emoji23][emoji23]
Huwa nasikia vibaya nikiyaona...au wwngine wanafunga kale kamkanda sehemu ya kuvutia gari..[emoji35][emoji35]
 
Kwahyo sisi wenye maduka ya urembo wa magari tutakula wapi?
Si kwamba tunaharibu biashara zenu...ila kuna aina ya urembo mnauleta, unafanya magari ya vijana yanakuwa kama majini...

Yaani kuna hawa vijana wadogo walioajiriwa jeshini, ukiona hizo IST zao na Rumion walivyozijaza maurembo, gari zimekuwa jini..[emoji35][emoji35]
 

Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?[emoji23]

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST [emoji119]

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue[emoji1787]
 
Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?[emoji23]

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST [emoji119]

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue[emoji1787]
Rumion ni gari nzuri nafikiri kwa toyota gari zake ndogo ndo gari nzuri kuliko zote. Rumion ni ist ama spacio sababu zina engine inayofanana. Ndio gari unaezasafiri nayo mbali kwa gharama nafuu.japo ulaji wake unazidi kidogo sana kwa spacio na ist na hii ni sababu ya umbile lake ambali linapingana na aerodynamics yenyewe haipenyi kwenye upepo bali inapingana nao. Ila utofauti wa ulaji huu ni negligble.
 
Mlimalizanaje na fundi mkuu??
 
Huwa nasikia vibaya nikiyaona...au wwngine wanafunga kale kamkanda sehemu ya kuvutia gari..[emoji35][emoji35]
Wengine wanakaweka karefu mpaka kanaburuza chini pamoja na clip kwenye kila corner ya bumper mbele na nyuma.
 
Hivi kuna siri gani wanajeshi wapya na Rumion?[emoji23]

Au ni maagizo kutoka juu

Yaani kama hajanunua Rumion basi premio/IST [emoji119]

Ili akaweke kale kamkanda,na fog light za blue blue[emoji1787]
Wale machalii ni ushamba wa kuigana...
Wengi wao ndiyo wana miaka 2 kazini..

Kazi ni kununua Rumion na kuzipimpu..[emoji2960]

Kisha apangishe single self, aweke flat screen kiubwa na mziki mnene...

Akimaliza hapo, kazi iliyobaki ni kula wake za watu...mtaani kwangu ndoa nyingi zimevunjwa na hivi hichalii..
 
Wengine wanakaweka karefu mpaka kanaburuza chini pamoja na clip kwenye kila corner ya bumper mbele na nyuma.
[emoji23][emoji23][emoji23]...huwa nashangaa wanataka nini..
Magaei yakianza matatizo, wansema gari flani huwa ni mbovu
 
Masoja wetu wengi wamepata bahati wamemaliza form four wakenda JKT wakapigika Mungu si athumani wakaitwa JW kwanini wasilinge , alafu hawana kazi tofauti na kwenda kazini kufyeka na kupasua kuni na saa 8 wanarudi nyumbani
 
Kwa kifupi, achana na kufanya modifications zozote kwenye wiring ya Nissan yoyote...
Haswa haya matakataka yanaitwa Android radio...
Mataa ya rangi rangi ndani mwngine yanawekwa mpaka chini ya siti..
Sheria ya kwanza ya kumiliki NISSAN. Keep it as close to OEM as possible. Maana yake wiring OG, spare OG.

Ila Dualis zina shida ya kiwandani. Firewall yake iko karibu sana na exhaust manifold, zile clip za plastic zikikatika zinailalia exhaust manifold na kwasababu inakuwa ya moto, inawasha. Ndio moshi mweusi huo nahisi.

NB firewall ni ile plastic inayokaa nyuma kwenye bonnet chini ya kioo kuzuia joto la engine kuja kwenye body/ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…