Nissan hardbody: Jeneza linalotembea.

Mr DIY

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2016
Posts
1,188
Reaction score
2,553
Kila mtu na kila siku tunakutana na hizi gari huko barabarani, makampuni, watu binafsi na hata taasisi za serikali wanatumia, je wanajua kuwa NCAP wamelipa score ya sifuri kwa kuwalinda walio ndani ya gari hili wakati crash hasa kugongana uso kwa uso, au hata ubavuni? Dhahiri hili ni jeneza linalo tembea.


Huu ni moja wa mifano ya crash tests za nissan hardbody 4x4 np300


 
Ili kujua gari si salama sana NCAP huwa wana test katika low speed, yaani chini ya 60km/h sasa kwa gari hii ni bora hata toyota passo iliyo score 3
Kwani unanunua gari kwa lengo la kugongana?

Kuna gari zinapewa score ya 100 ila zikipata mzinga unakata ringi hapohapo.

Endesha kwa usalama na tahadhari muda wote.
 
Mtoa hoja umetoa hoja bila kuchimbua kwa undani...

Hiyo Nissan Hardboard NP 300 nyeupe ni Toleo maalumu kwa nchi masikini za Africa..

hiyo nyeusi ni toleo la ulaya...

Umasikini wetu wa kiafrika na kupenda vya kunyonga ndiyo unaofanya tuletewe vitu vyenye ubora wa chini..

Kampuni ya Nissan hapo hawana kosa, kosa ni umasikini wenu...

Hao Nissan nao ni wafanga biashara, wakisema watutengenezee kwa standard za Europe, waafrica mtakimbia.....

Ni sawa na Tecno,Itel au Infinix....huu uchafu umewahi kuuona soko la Ulaya, America au Canada..?....Hizi ni smartphone maalumu kwa kundi masikini la Africa.

Kabka hujaandika, angalia kwanza unaishi pande zipi za dunia...NP 300 unazoziona huku, haziuzwi soko la Ulaya wala America....
 

Suala la usalama ni muhimu hasa ukizingatia kwamba mtumiaji wa barabara si wewe peke yako. Hivyo hata kama utajitahidi kuendesha gari vizuri kwa tahadhari bado unaweza ukapitiwa na mtumiaji mwingine wa barabara na yakawa majanga kama kawaida.

Bado gari lenye score ya 5 linakuwa na uwezo mkubwa wa kulinda Occupants kuliko gari lenye Score ya 0.

Hizo gari hazifanani kwenye usalama.
 
Kwani unanunua gari kwa lengo la kugongana?

Kuna gari zinapewa score ya 100 ila zikipata mzinga unakata ringi hapohapo.

Endesha kwa usalama na tahadhari muda wote.

Shida ni moja. Barabara hautumii peke yako. Unaweza ukaendesha kwa tahadhari ila mwenzako akawa yupo Rough na akakupitia.

Hivi unajua ni kwa kiasi gani airbag mbili tu zile za mbele zimepunguza vifo vinavyotokana na ajali?
 
Maisha ni kuchagua, ni bora mnunuzi awe na taarifa na product anayoinunua kuliko kuto jua akidhania yupo salama
 

Sahihi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…