Wakubwa nimenunua gari aina ya nissan xtrail mwaka 2022 mwezi Nov aina ya engine ni MR20 nafikiri kwa wazoefu wa gari engine yake haina tofauti na engine ya nissan dualis ,, nilichoshangaa toka mwaka jana mwezi kama wa kumi gari ikaanza kama kushtuka shtuka hivi hasa nikipinguza mwendo mpaka kwenye 40km/h yani hata nikiwasha na kuanza kuondoka ikifika kwenye 40km/h to inaanza kushake shake yani kama inamissi hivi [ jerking action] fundi akanishauri nibadili plug kwani toka ninunue gari sijawahi badili plug nilivyobadili ikatulia kama week moja hivi ikaanza tena nikamshirikisha fundi mmoja huko dar akasema hizo gari saiz zinachagua sana plug inabidi uweke plug oG akasema kunasehem tunaagiza nje weka oda nikaweka hiyo oda ambazo zimenigharim 400k , zilipokuja nikafunga gari ikatulia kama mwezi hivi nashangaa juzi tena hali imerudia ile ile , nimebadili hydraulic wapi na kwenye dashboard hamna warning light yoyote ile ,, naombeni msaada wenu wakubwa .