Nissan X-Trail

Mkuu uwe unaweka na mawasiliano kabisa ili watu wakupe kazi.
Hbr za leo kaka,

Asante kw wazo hilo. Mawasiliano yapo, kw. mfn. waeza nifata inbox ili kupatana vizuri kuhusu kazi.
 

Bro hilo group limefikia wapi
 
Habari za Leo, nahitaji kununua brake pads na CV joints za Nissan Xtrail NT31 ambazo ni nzuri, nitazipata wapi?, na bei zikoje?
 
Habari za Leo, nahitaji kununua brake pads na CV joints za Nissan Xtrail NT31 ambazo ni nzuri, nitazipata wapi?, na bei zikoje?

Kariakoo duka linaitwa Master card karibu na salama bearing huyu ana spare originally za nissan
 
Naomba kujua shokup za nissan Xtrail 2005, inaweza kuwa bei gani mpya
 
Bro. Ofisi zako ziko wapi?
 
Mkuuuu weka Mawasiliano Yako Tukutafute. Unatoa Madini mpaka Raha Yani. Daaaah we Jamaaa unajua mpaka kero yani.. Hongera Bro.
 
Yani, mimi nina Nissan Xtrail 2008, nimeiagiza Juzi tu. But nimesikia watu wengi wanaziponda sana, na wengi wanalalamika kwamba hizi Gari tatizo Lake kubwa ni Ku chemsha. Sasa mimi ndo kwaaanza nimeanza kulitumia. Naogopa hili tatizo lisije likanitokea. Sasa nawaza ni precautions gani Nichukue ili gari langu lisije likapata hili tatizo la kuchemsha.
Kuna watu wananishauri nichomoe Thermostart ili maji yawe yana flow directly, alafu niongeze Njia kwenye Rejeta, lakini sasa naogopa je inaweza athiri mfumo wa Gari.? Naweza itumia hivi hivi bila kuathiri mfumo wake wa awali? What precautions should I take.? Naomba unishauri Mkuu, Asante sana
 
Naomba nikuambie kitu, japo najua wenye Toyota zao watakuja kupinga, siwakatazi kupinga kwa sababu kila mtu ana uhuru wake...

Sikushauri utoe thermal start kama watu wanavyokushauri....Mjapan aliyeiweka si mjinga.

Hizo habari za kwamba Xtrail zina ugonjwa wa kuchemsha ni MYTHS tu ambazo watu wamekuwa wakiamini kwa sababu..

Nissan xtrail huwa halitaki kuweka maji ya bombani kwenye radiator, wabongo tunapenda urahisi wa mambo...unakuta mtu anamiliki vitz anaweka maji ya bombani, basi na kwenye x ttail anafanya hivyo....x trail iwekee coolant iliyopendekezwa... coolant hupooza gari kwa kiwango kinachotakiwa tofauti na maji ya bomba, kisima au mtoni.

Weka engine oil iliyopendekezwa na mtengezaji sana sana iwe 5w 30...kibongo bongo tunaamini zaidi Castrol au Total.....kumbuka oil mbali na kulainisha injini, pia hupooza injini..

Mara kwa mara hakikisha kiwango chako cha coolant hakishuki below the minimum level.

Kuna watu wapo wanamiliki x trail zaidi ya miaka 6 sasa, wameshafanya nazo masafa karibu mikoa yote na nje ya nchi mfano Kenya, Uganda bila kufanya modifications zozote kwenye engine....

Ingekuwa haya magari ni mabovu kama watanzania wanavyosema, Nissan Motors Corporation Japan wangeshasitisha uzalishaji wake...ina maana ni gari zinazofanya vizuri ndiyo maana uzalishaji wake unaendelea na sasa Nissan Xtrail wapo Generation ya tatu kama sikosei...

Mafundi wa Tanzania hawataki kusoma, wamezoea mifumo ya Toyota, hivyo wao ndiyo chanzo kikubwa cha kuwakatisha watu tamaa kwa upande wa xtrail....
Sisi watanzania ni watu wa ajabu..mtu akishindwa kitu hataki kukubali, anakiponda...mafundi wengi x trail zinawatoa jasho, kwa hiyo wanawadanganya watu hizi gari hazitengenezeki....

Kwa ninj zisitengenezeke, gari lina OBD, ni kiasi cha kusoma code na kuitafsiri inaashiria nini, then you do a replacement

Chonde chonde, x teail usiipeleke kwa mafundi makanjanja, mwembeni...ukihisi tatizo weka vipimo vya computer, replace parts with genuine ones......hapo x trail utaiendesha miaka 8 bila kujuta.
Siku zote usichukue experience ya utunzaji wa Toyota ukaihamiahia kwenye X trail..hapo utateseka...

Mwisho.....gari ni matunzo kwa kuzingatia instruction manul yake.....na si kwa kuzingatia maneno ya watanzania.
 
Sidhani kuna lolote la kuongezea hapo juu
 
Mkuu inaelekea wewe una nissan kama hutojali na upo Dar toa mawasiliano ya mafundi wazuri wa nissan utakuwa umesaidia wengi sana
 
Mkuu inaelekea wewe una nissan kama hutojali na upo Dar toa mawasiliano ya mafundi wazuri wa nissan utakuwa umesaidia wengi sana
Yes mkuu... nina NISSAN ila nipo Arusha...
 
Mkuu inaelekea wewe una nissan kama hutojali na upo Dar toa mawasiliano ya mafundi wazuri wa nissan utakuwa umesaidia wengi sana
Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu?
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.
Au coolant yoyote ile basi inafaa?
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ?

Asante
 
Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu?
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.
Au coolant yoyote ile basi inafaa?
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ?

Asante
Mkuu sina gari hiyo ila nina uzoefu nayo kwa kuwa kuna ndugu yangu anayo na huwa naitumia mara kwa mara. Coolant inayotakiwa ni hiyo hapo chini. Aidha kumbuka xtrail ina engine parts ambazo ni aluminium hii ina maana kuwa ukichakachua coolant ukaweka ambayo haina viwango vinavyotakiwa basi ukipata majanga usilaum mtu na kumbuka Nissan Xtrail zina kawaida ya kuoverheat sanaaaaa incase hujafuata masharti yake. Kama upo Dar nenda duka linaitwa Mastercard, DT Dobie au kisangani utapata coolant original.

Summary
Je nitaijuaje coolant inayotakiwa kwenye nissan xtrail yangu? Jibu Cheki manual ya gari lako zipo online au cheki picha chini
Naomba jina la ya coolant unayotumia wewe kwenye xtrail yako.Jibu Cheki manual ya gari lako zipo online au cheki picha chini
Au coolant yoyote ile basi inafaa? Jibu HAPANA weka ambayo NISSAN wamesema uiweke usijaribu kuweka nyingine
Au lazima niende nunua coolant kwa Nissan authorized agent ? Yes ili kuwa na uhakika halafu why ununue gari around 15M then uone ubahili kununua coolant nenda DT Dobie au Master Card au Kisangani ingawa nadhani Master Card bei yao itakuwa cheap kuliko hao wengine

 
Shukrani mkuu
 
Habari wadau, nina Nissan xtrail ya mwaka 2008. Ikifika speed kati ya 40 na 60 gari inavuma sana na kuanza kutetemeka. Ila nikivuka hadi 80 mvumo unapungua kidogo. Je tatizo laweza kuwa nini?
 
Huu uzi potential sana, nina mpango wa kuagiza Nissan X trail Axis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…