Hii ni Xtrail ya 2007/8. Taa ya check engine inawaka lakini gari inafanya kazi vizuri tu. Nimejaribu procedure za kui-reset lakini bado. Pia nilichomoa battery kwa sekunde chache lakini bado. Kuna jamaa yangu kaniambia yeye inawaka mwaka wa pili sasa na maisha yanaendelea kama kawaida. Kasema kama kungekuwa na tatizo gari isingekubali kuwaka. Ila mimi sijisikii salama hiyo taa ikiwaka. Kama kuna fundi mwenye machine ya kucheki Nissan Xtrail maeneo ya Mwanza, tuwasiliane. Au kama kuna msaada wowote namna ya kuizima (reset) hiyo taa.