Nitabaki na mke wangu na wanangu, kumbe ndugu ni kenge tu

Jf tunafanywa kama watoto, huyu mtu kuna uzi wake anaomba ushauri ya kwamba mume wake kamtukania mama yake.


Daa hii inatisha
Kwani hawezi vaa uhusika wa mtu mwingine?

Usikariri...
 
Dual zangu zoote siku zote ni kumuombea Mume wangu afya njema na maisha marefu tulee watotowakue vyema tuzeeke wote,maana naona ukoo ule ulivyokuwa na makucha makali endapo mwenzangu atatangulia woooi ee Mungu nitunzie mm..imagine mtu ako na above 40 something bado anamtegemea mdogo ake kwq kila tatizo linaloopata familia yake ,na ni yeye peke yake alofanikiwa katika familia among 5 wote wanamtegemea na jiwatu wazima na familia zao..uziuri ni kwamba hata yy anajua endapo itatokea hivo nn kitafafuata.
 
hahahahaa haya mambo yaanchanganya sana sana, leo aankua mwanaume, kesho anakua mwanamke.....umeweka mambo vyema
 
Hongera sana, yaani kutoka kwenye kuumwa mahututi hadi kukopa na juzi tu ukatoka hospital December leo hii January 5, 2024 una mabulungutu yote hayo, na ukapata na nguvu kabisa za kuendesha gari hadi kwa Dada yako, ukatapa na nguvu za kumtishia panga? Mental Problem is real kimtindo
 
ndugu ni karume kenge
 
Pole sana. Ndugu sio kabisa. Mke ndio kila kitu hapo. Hakika MUNGU akakupa mtihani ili uwajue vizuri.
Nimejifunza kitu hapa. Nabadilika soon.
 
Kwa nini akili za wanawake wa Kibongo huwa mnawaza mwanaume ndio aanze kufa?
 
Mkuu kwenye maisha unapomsaidia mtu usitegemee chochote hata yesu aliponya watu wengi ukoma ila ni mmoja tu ndio aligeuka nyuma na kushukuru hao ndio binadamu walivyo expect nothing to them.
Mkuu angekuwa ni mke ndio amefanya hayo kwa mumewe ungeandika hivi
 
Pole chief, sometimes ndugu ni viazi sana.. labda mama yako mzazi tu ndo anaweza kua mwema kwako, lakini ndugu wa kawaida mpaka baba yako mzazi anaweza kukupiga tu kwa hali yoyote ile
Hata huyo mama usimwamini.
Labda useme huyo wa kwako hajawahi kupigwa matukio.
 
Kwa nini akili za wanawake wa Kibongo huwa mnawaza mwanaume ndio aanze kufa?
Sasa mwanamke hata akitangulia kufa unataka amuachie nini mwanaume, ni familia ngapi ambazo mama akitangulia utakuta migogoro ya mali, kulinganisha na zile ambazo ametangulia baba

Hilo linajulikana ikitokea mama katangulia haitaleta shida, sababu baba ana uwezo wa kusimama kiuchumi na kuendelea kuwatunza na kuwahudumia watoto, hivyo hilo suala tayari lina suluhisho lake

Sasa mtihani unabaki pale ambapo atatangulia baba, hili ndilo suala ambalo mara nyingi linakosaga suluhisho kwenye familia zetu za kiafrika na kuleta migogoro, ndio maana watu wamekomalia hilo tu
 
Wewe umesema ndugu zako hawana mbele wala nyuma wewe ndio mwenye nafuu sasa watoto wako wangepelekwa kwa Baba Mdogo wangeweza kula mihogo mitupu bila dagaa wala maharage?

Ni kweli ulikuwa unaumwa lakn hata hivyo wewe kimaisha una nafuu kuliko ndugu zako makabwela ambao ni wazima.

Ukumbuke dunia hii kuna watu kitu pekee cha thamani walicho nacho kwenye maisha yao ni Uzima tu. Hawana Mbele wala nyuma ukitegemea msaada kwa watu kama hawa basi ujue unajiandaa kuwalaum tu maana theu have nothing to offer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…