Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari , ninapenda sana kupika mandazi, sambusa n.k ila nikishaivisha mandazi yanakua yamenyonya mafuta mengi sana, na ndani yanakua hayana nyama. Ninaomba mnijulishe nifanyaje ili yatoke vizuri bila kunyonya mafuta mengi na kukosa nyama.
Asante.
Lateni sielewi unakosea wapi, ila katika experience yangu huwa naona baadhi ya vitu ambayo husababisha maandazi kunyonya mafuta ni kukosea wakati wa ukandaji wake. Baadhi ya sababu ni kukandia mafuta mengi, kutoweka kabisa amira (iwe baking powder ama yeast a.k.a amira ya chenga); na pia tabia ya kuyakaanga kwenye moto mdogo mno katika mafuta ambayo bado ni mabichi.
Kama hapa hujanielewa na kupata suluhu, tafadhali naomba process yako ya ukandaji hadi upishi ili kuelewa tatizo lipo wapi.
Mimi huanza kwa kutia sukari kidogo, iliki, hamira, na ninakandia maji ya uvuguvugu,wakati wa kukanda siweki mafuta, nikishamaliza kukanda, ninayakata na kuyaacha yaumuke , then ninaya kaanga,
nahisi tatizo langu liko hapo kwenye moto mdogo na mafuta mabichi, pia mdau Dora amenishauri niwe naweka chumvi kidogo .