Nitaiburuza serikali mahakamani kama nilivyoahidi

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Mimi nipo kuwatetea Watumishi wa Umma. Hawa ni walimu Madaktari, wauguzi, manesi nk. Hawa ni watu muhimu sana katika jamii.

Katika mikataba yao ya kazi kuna kipengele kinachosomeka "Your incremental date will be on July 1st", yaani kila mtumishi wa Umma atapata nyongeza ya mshahara ya mwaka kila tarehe 1, July.

Kwa makusudi serikali imekuwa ikivunja masharti ya mikataba ya watumishi wa Umma bila kujali chochote.

Lakini pia upandishaji madaraja kwa watumishi wa Umma hauzingatii nani aanze kisha afuate nani. Hivyo utakuta watumishi walioanza kazi kwa kupishana miaka hata 8 wote wanakuja kuwa kwenye daraja moja kitu ambacho si kizuri.

Kwa sababu hizo, nitaipeleka mahakamani serikali ili haki iweze kupatikana kwa watumishi wa Umma.
 
Rais wetu ameshasema kabisa kuwa anaweka msawazo kwa mserereko kwa walimu

Na baadhi ya halmashauri bado wanaona hiyo sio muhimu ila inaumiza sana mtu mmeanza pamoja halafu unakuta mwenzako kakuzidi zaidi ya madaraja mawili

Kwakweli inauma sana na tunamwachia Rais aone namna ya kuwasaidia walimu wake
 
Hongeza HOJA nyingine,Kulipia LESENIi ya utendaji kazi Kila mwaka Kwa gharama kubwa Kwa fani km nurses,udaktari huku hawafanyi biashara na KUTOPANDISHWA MADARAJA km mtumishi Ambaye hajapata Leseni japo alijiendeleza(Tena Kwa gharama zake mwenyewe)ni unyanyasaji mkubwa Kwa WATUMISHI ,
 
Mimi nipo kuwatetea Watumishi wa Umma. Hawa ni walimu Madaktari, wauguzi, manesi nk. Hawa ni watu muhimu sana katika jamii.

Katika mikataba yao ya kazi kuna kipengele kinachosomeka "Your incremental date will be on July 1st", yaani kila mtumishi wa Umma atapata nyongeza ya mshahara ya mwaka kila tarehe 1, July.

Kwa makusudi serikali imekuwa ikivunja masharti ya mikataba ya watumishi wa Umma bila kujali chochote.

Lakini pia upandishaji madaraja kwa watumishi wa Umma hauzingatii nani aanze kisha afuate nani. Hivyo utakuta watumishi walioanza kazi kwa kupishana miaka hata 8 wote wanakuja kuwa kwenye daraja moja kitu ambacho si kizuri.

Kwa sababu hizo, nitaipeleka mahakamani serikali ili haki iweze kupatikana kwa watumishi wa Umma.
Ni jambo jema ila ninakuuliza hao unaotaka wapate haki zao wanakubaliana na wewe? Au watakuona unania ovu ya kuwagombanisha na mama! Usije ukashangaa watakapokukana, ninakushauri usijaribu kumtetea mtanzania atakuumbua.
 
Mimi nipo kuwatetea Watumishi wa Umma. Hawa ni walimu Madaktari, wauguzi, manesi nk. Hawa ni watu muhimu sana katika jamii.

Katika mikataba yao ya kazi kuna kipengele kinachosomeka "Your incremental date will be on July 1st", yaani kila mtumishi wa Umma atapata nyongeza ya mshahara ya mwaka kila tarehe 1, July.

Kwa makusudi serikali imekuwa ikivunja masharti ya mikataba ya watumishi wa Umma bila kujali chochote.

Lakini pia upandishaji madaraja kwa watumishi wa Umma hauzingatii nani aanze kisha afuate nani. Hivyo utakuta watumishi walioanza kazi kwa kupishana miaka hata 8 wote wanakuja kuwa kwenye daraja moja kitu ambacho si kizuri.

Kwa sababu hizo, nitaipeleka mahakamani serikali ili haki iweze kupatikana kwa watumishi wa Umma.
Waalimu wasiongezewe mishahara daima! Wanashiriki kuipora haki ya wananchi kuchagua viongozi na watawala kwenye hi nchi. Hali inayopelekea na wao kuwa na maisha magumu kama sisi. Waangamie kabisa hawana Maana.
 
Kwa sababu hizo, nitaipeleka mahakamani serikali ili haki iweze kupatikana kwa watumishi wa Umma.
Mkuu kesi ya mbuzi huwezi kupeleka buchani,
:muulize hans patoon a.k.a Andrew wa mwalimu nyierere
analindwa na watu asiotaka wamlinde.
Juzi hapo wamemfata huko kwao kijijini kawakimbia.
 
Sisi walimu wa tz tunamaisha mazuri.wewe mleta mada acha kufungua ki kesi chako uchwarwa
 
Rais wetu ameshasema kabisa kuwa anaweka msawazo kwa mserereko kwa walimu

Na baadhi ya halmashauri bado wanaona hiyo sio muhimu ila inaumiza sana mtu mmeanza pamoja halafu unakuta mwenzako kakuzidi zaidi ya madaraja mawili

Kwakweli inauma sana na tunamwachia Rais aone namna ya kuwasaidia walimu wake
Watumishi sio walimu tu kada zote za utumishi hta jw,police, utendaji, Os wote hao watumishi
 
Mimi nipo kuwatetea Watumishi wa Umma. Hawa ni walimu Madaktari, wauguzi, manesi nk. Hawa ni watu muhimu sana katika jamii.

Katika mikataba yao ya kazi kuna kipengele kinachosomeka "Your incremental date will be on July 1st", yaani kila mtumishi wa Umma atapata nyongeza ya mshahara ya mwaka kila tarehe 1, July.

Kwa makusudi serikali imekuwa ikivunja masharti ya mikataba ya watumishi wa Umma bila kujali chochote.

Lakini pia upandishaji madaraja kwa watumishi wa Umma hauzingatii nani aanze kisha afuate nani. Hivyo utakuta watumishi walioanza kazi kwa kupishana miaka hata 8 wote wanakuja kuwa kwenye daraja moja kitu ambacho si kizuri.

Kwa sababu hizo, nitaipeleka mahakamani serikali ili haki iweze kupatikana kwa watumishi wa Umma.
Cha kushangaza zaidi utashambuliwa na walewale unaowatetea
 
Sisi walimu wa tz tunamaisha mazuri.wewe mleta mada acha kufungua ki kesi chako uchwarwa
Nikweli kabisa mnamanisha mazuri. Cha ajabu mmelalamika kutozwa 50k ya mwenge.

Pia ninyi hapohapo mlimchangia Samia Hela akachukue form.

Trh 25 mwezi huu mwalimu kapigwa kama Ngoma kisa ana madeni lukuki
Maisha magumu.

Ingia pm nikuunganishe nae umsaidie mwalimu mwenzako maana anawaabisha huku ninyi mnasema mnamaisha mazuri welele
 
Walimu wataandamana kukupinga, na kukutaka usiwagombanishe na serikali sikivu ya Rais wao mpendwa, jemedari wa vita, mpambanaji wa haki na maisha bora ya walimu anayewafanya kila siku wabubujikwe na machozi ya furaha, aliyewafanya walimu wa Tanzania kuwa kwenye maisha bora kuliko walimu wote Duniani.

Na risala hiyo itasomwa na mzalendo sana wa CCM, ndugu Lucas Mwashambwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu shetani hana bando tangu Jumamosi
 
Back
Top Bottom