President Elect
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 693
- 212
Nikiwa mwanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi mwenye kadi# natamka bayana kuwa nitaitumia vema haki yangu ya kikatiba kuipigia kura ya HAPANA katiba inayopendekezwa. Kuwa mwana CCM hakuninyimi utashi wa kufanya maamuzi sahihi kwa taifa letu, nitasema kweli daima! Nawaomba sana wana CCM wenzangu wenye uchungu na taifa letu mniunge mkono!
Mapinduzi ya kweli yataletwa na wana CCM ndani ya CCM. Jamani tusiwe vipofu, nchi yetu inaangamia mikononi mwetu tungali tunaona, tuchukue hatua kabla jua halijazama!!!
Kura ya HAPANA kwa katiba inayopendekezwa, ndio jibu sahihi la katiba hiyo kuboreshwa ndani ya siku 60 kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba!