Nitajaribu kutunga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
1.Mwenye wivu jiandae,mkola nagawa kamba
Donda dugu sikomae,niwakomoe manamba
Wachutame na wakae,nikiwasomesha namba
Nitajaribu kughani,asopenda ajinyonge.


2.Daima siwezi acha,jambo ninalolipenda
Nakwona unavyo kacha,kwa mambo ninayotenda
Nongea lugha ya picha,vipi watokwa udenda
Nitajaribu kughani,wanelewa kiserema ?


3.Kumbe Hata wewe nobe,sisemi kwamba naringa
Ila kumgusa Kobe,ni sheria kuipinga
Nadhani nawe ni zobe,mbona unazinga zinga
Nitajaribu kughani,nijenge yangu sauti.


4.Elewa Mimi si mango,sauti ninaipanga
Si yako kama ya pango,ianzishayo kisanga
Mbona hujafuta tongo,kabla ya kwanza kutunga
Nitajaribu kughani,kwa sauti nipendayo.


5.Eti niache kughani,huko nanze kujitenga
Niishie kitabuni,si sheria za malenga
Labda ni za kizamani,sasa vyote ni kulenga
Nitajaribu kughani,moto wake sitozima.


6.Rasmi ninakupa kamba,tukisubiri matanga
Jinyonge ewe mshamba,miye nalishusha tanga
Baharini nina tamba,baki una mangamanga
Nitajaribu kughani,hadi kije eleweka.


SHAIRI-NITAJARIBU KUGHANI.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…