Binafsi naamini kwa kula mlo kamili tunapata mpaka afya ya ubongo. Tunakuwa uwezo mzuri wa kufikiri. Kula hovyo kunaweza kupelekea hata kupata magonjwa badala ya kupata afya! Waafrika tuna haki pia ya kula vizuri! Inawezekana sikula vizuri hapo kabla lakini natamani sana wanangu wale vizuri wapate afya na akili pia. Ahsante kwa mchango wako!
Jitahidi sana kulimit sehemu wanazokula, hakikisha watoto wanakula nyumbani na si sehemu nyengine Kama hakuna sababu ya kufanya hivyo. hii itakupa uhakika wa kile wanachoandaliwa kua ni salama na chenye faida kwa afya ya mtoto.
Epuka sana fast foods, haziongezi chochote zaidi ya calories na risks za kupata magonjwa mabaya.
Muhamasishe mama watoto awatengenezee healthy treats nyumbani ili wanapopata hamu ya kutafuna tafuna watafute snacks zenye faida, watoto wanapenda rangi, mnaweza kudesign matunda kwa kuchanganya rangi ikawa kivutio kwao.
Usisahau miongoni mwa vyakula muhimu sana kwa watoto:-
Maziwa,
cheese(jitahidi upate genuine brand Kama uwezo upo mfano kiri , al marai ),
salmon,
sardines,
Parachichi,
Carrots,(hizi unaweza ukawazoesha wakawa wanatafuna Kama snacks)
Biringanya,
ufuta nk.
Vipo vingi sema hakikisha vile unavyoweza kumudu unawapa watoto Mara kwa Mara.
Kataa vitu Kama soda, jus cola and likes, pipi, biskuti, chama and other funny names kuingia ndani ya nyumba yako wala kupewa watoto wako, fanya iwe sheria itasaidia somehow kupunguza au kukata matumizi ya hivyo vitu.
We're what we eat......ukiangalia sana kuhusu hili athari yake ipo moja kwa moja kwa vijana wetu wa tunaokula sembe na kachumbari....uwezo wao wa kufikiri unafifia mno as days goes on....hawawi critical thinkers na wanabehave in very annoying manners, pamoja na utandawazi, lishe duni inachangia kwa kiasi kikubwa sana kuwabomoa...........
majanga yanakua mengi kwa sababu watu hawazinourish akili zao ziwe kwenye optimum level ya matumizi.
Wazee wetu walikua bora kwa sababu wao walikua na access na chakula asili na katika ubora wake.....wazungu na jamii nyingi nje ya Africa mpangilio wa chakula ni utamaduni unaoheshimiwa na kurithishwa kwa hiyo watoto wanakua wakiwa na uelewa na nidhamu kuhusu eating habits.