Nitakuwa wa mwisho Kuuamini huu Upuuzi ambao naona Simba SC yangu wanaanza kutaka Kuutumia kama sababu ya Kushindwa

Nitakuwa wa mwisho Kuuamini huu Upuuzi ambao naona Simba SC yangu wanaanza kutaka Kuutumia kama sababu ya Kushindwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mimi ni Simba SC damu ila sijazoea Unafiki, Ujinga na Upumbavu na nitakuwa wa mwisho pia Kuuamini. CAF kubadili Waamuzi wa mchezo Kwangu Mimi si hoja kwamba Simba SC tunahujumiwa na nimeshtushwa pia kumuona Mwanasimba mmoja ambaye pia ni Mbunge na Mwanasiasa nae bila haya / aibu akiingia katika Upuuzi huu.

Hivi ni mara ngapi hapa hapa katika Ligi Kuu yetu Simba SC huwa tunabadilishiwa Waamuzi? Je Timu pinzani huwa zinatulalamikia kwa TFF? Kama tunadai kuwa hatua hii ya CAF ni ya Kuihujumu Simba SC yetu Sisi Simba SC tulishindwa nini nasi Kuwahujumu vilivyo ile majuzi?

Hivi TP Mazembe ndiyo waliifanya Miguu ya Nahodha Wetu John Boko ilione lango lipo juu akapaisha kule badala ya Kulilenga vyema? Hivi Simba SC nani alitufanya tushindwe kuzitumia zile ' clear chances ' tulizozipata matokea yake Wachezaji wetu wakawa wanarukaruka tu kama Maharage ya Mbeya?

Simba SC msitake kuwafanya Watanzania hasa Mashabiki wetu ( GENTAMCINE nikiwemo ) kwamba ni Wajinga au Wapumbavu au labda wengine hatujawahi Kucheza mpira au hatujui Kuuchambua vile vile. Hivi kuna nani hajui kuwa Simba SC hata kama hao Waamuzi wasingebadilishwa hivi bado Kuwafunga TP Mazembe Kwao Lubumbashi ilikuwa ni ngumu?

Hivi mmejua kuwa kwa Kitendo chenu hiki cha Kulalamikia Mabadiliko haya ya Waamuzi tayari Kiufundi mmeshawaharibu Wachezaji wetu Kisaikolojia? Mimi naamini kuwa kama Simba SC ikijipanga vyema kabisa pamoja na CAF kubadili hao Waamuzi bado tunaweza Kuwafunga TP Mazembe huko huko Kwao.

Uwezo wa Wachezaji wa Simba SC hasa hawa tulionao siyo wa Kushindana na Vilabu vikubwa na hata hii kufikia tu hapa ni Bahati tu ya Mwenyezi Mungu hivyo tusitake kujifanya kama vile Sisi ni Timu bora na ina Mapafu ya Kushindana na hawa Majabali wakubwa wa Kimpira Afrika.

Mkiambiwa kuwa tumieni vizuri Uwanja wenu wa Nyumbani muwe mnaelewa na nadhani mmewaona Mamelodi Sundowns walichowafanya Al Ahly hadi wakawafunga zile Goli Tano kwa Nunge ( 5 - 0 ) wakati Sisi huku Kipaumbele chetu Kikuu kikiwa ni Kuujaza tu Uwanja na kuwa na Tiketi za ' Platinums ' za Kutosha.

Najua wana Simba SC wengi kwa Uzi huu leo mtanichukia GENTAMYCINE ila huwa silei Ujinga na Upumbavu na Unafiki Kwangu ni mwiko bali nitakuwa nanyoosha tu pale ambapo naona panabidi kufanywa hivyo. Ushauri pekee ambao nautoa ni kwamba nawaomba Wachezaji wazawa wa Simba SC kama Mdogo wangu Mkude akina Ndemla, Tshabalaa, Dilunga na Muzamiri wautumie huu mchezo kama sehemu yao ya Kujiuza ili ikiwezekana basi TP Mazembe au Vilabu vingine vikubwa viwamulike na kuwasajili ili Tanzania iongeze idadi ya Wachezaji wake wanaocheza nje.

Ni Mpumbavu tu pekee na asiyejua Mpira vyema ndiyo alikuwa anajua na kujiaminisha kabisa kuwa eti Simba SC ina ubavu / uwezo wa Kumfunga TP Mazembe Kwao ' Machinjioni ' huko Lubumbashi. Twendeni tu tukapokee Magoli yetu ya Kutosha ili yatutie Ndimu / Hasira na tukirudi sasa Hasira zetu zote tuzihamishie katika Mechi zetu za Viporo na zile za muendelezo wa Ligi Kuu ili tulichukue tena hili Kombe kisha Mohammed Dewji na Kamati ya Usajili ya Simba SC bila kusahau benchi la Ufundi likae chini na lifanye Usajili ' Kabambe ' kwa ajili ya Michuano ijayo ya CAF Champions League ambayo GENTAMYCINE naamini kuwa kama Simba SC itashiriki tena na Kusajili ' Majembe ' ya maana basi kwa Msimu ujao tunaweza hata kufika Fainali na kwa Kudra zake Mwenyezi Mungu hata Kuchukua Kombe.

Tuacheni kutafuta Visingizio vya Kipuuzi vya Kulalamika Waamuzi Kubadilishwa. Na hapa nimewadharau Kidogo Viongozi wangu mtanisamehe sana katika hili. Cha kufanya tu sasa badala ya Kulalamika kubalishiwa hao Waamuzi nadhani tutumie tu muda huu Kuwaandaa na Kuwajenga vyema Kisaikolojia Wachezaji wetu kuwa wakiona Magoli yanaingia mfululizo kwa Golikipa Aishi Manula wasiwe wanashangaa bali wajue tu ya kwamba hao ndiyo TP Mazembe na hapo ni ' Machinjioni ' Lubumbashi.

Nawasilisha.
 
Huyo mwamuzi ametoka kutumikia azubu yake af anakuja kuchezesha mech ya simba azubu yenyewe ni kupokea rushwa
 
Ni kweli kabisa waamuzi huwa wanabadilishwa lakini hiyo haiondoi haki ya timu kulalamika!
Huyu mwamuzi alipata kashfa mwaka jana kwenye mechi ya nusu fainali kati ya Esperance de tunis vs premera de agosto kafu wakamsimamisha kuchezesha lakini baada ya kugundua hausiki na hujuma za Esperance amefunguliwa.
Kumbuka huyu mwamuzi mwaka 2016 alichezesha fainali ya vilabu duniani nchini Japan kati ya Kashima antlers Vs Real madrid pia mechi ya world cup kati ya Belgium Vs panama yuko vizuri!
Hii mechi aliyopewa ni kawekwa kikaangoni yupo kwenye blacklist ya CAF akifanya madudu tu hatunaye tena.
Wewe unaitwa Fala, mjinga, boya na wadau kwa sababu uwezo wako wakufikiri ni mdogo kaka! Simba wanayohaki yakulalamika japo haitobadili chochote yule mwamuzi anatokea Ndora ni karibu na Lubumbashi na hata makabira yanaingiliana!
 
Wewe ni lofa. Kwanini wasilalamike??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sipotezi muda na Watu walioanza Kuujua na Kuufuatilia Mpira wa Miguu pale Jose Mourinho alipoibuka na kuwa Kocha wa Chelsea tafadhali. Huna ubavu wa Kujenga Hoja na Mimi hasa katika Medani hii ya Mpira kwani achilia mbali tu Kuuchambua na Kuujua pia nimeucheza sana tu na pengine isingekuwa Ukali wa Wazazi na kutaka nijikite zaidi katika Masomo na kutopenda Mtoto wao niwe Mchezaji enzi hizo kuna uwezekano GENTAMYCINE ningekuwa nimeshamtangulia Mbwana ' Popa ' Samatta Siku nyingi mno huko Ulaya ( Ng'ambo ) Siku ukipata muda uwe unatembelea Viwanja vya Barafu au Garden uwe unaona ninavyofanya vitu vyangu hasa sehemu ya Kiungo au Beki Mbili na Tatu. Karibu sana!
 
Kwa ' Great Thinker ' kama Mimi hii ni Hoja dhaifu kabisa. Msinilazimishe nikaanza Kuwadharau tafadhali.
 
Kwa ' Great Thinker ' kama Mimi hii ni Hoja dhaifu kabisa. Msinilazimishe nikaanza Kuwadharau tafadhali.
Ndugu weka hoja zako zinazopingana na zangu nimeweka mpaka details zangu kuonyesha ni jinsi gani naufatilia mpira! timu zina haki ya kulalamika haijakatazwa ila wanaopanga waamuzi ndiyo wanamamlaka ya kupanga ama kupangua referee tena bila hata sababu CAF wao wapuuzi wamejiwekea mtego wenyewe eti sababu ya kiufundi😡 hapo tutahitaji ufafanuzi zaidi
 
Mzee Baba GENTA usiogope hizo ndio zinaitwa figisufigisu za soka,ukipata mwanya unapenyeza mpaka panatanuka unafanya yako!!Tunawajambisha tu wakiruka tunajua zimo

Sent using Jamii Forums mobile app

Tunaacha Kulaumu, Kujilaumu na Kutafakari kwanini mechi yetu ya Juzi ' Kwa Mkapa ' tumembwela mbwela tu hadi Kushindwa Kuwafunga TP Mazembe sasa hivi tumerukia CAF na sababu ambayo GENTAMYCINE sioni aibu Kuiita ni ya Kipumbavu kabisa kuwa kwanini Waamuzi wamebadilishwa na cha Kushangaza kuna Watu wengi tu nao wanaamini kuwa hapa Simba SC imehujumiwa lakini hao hao wakati Timu yetu ya Simba SC ikiwa inacheza hapa TPL na Waaumuzi wa mechi Kubadilishwa ili watubebe wala masikini ya Mungu Timu Pinzani huwa hazilalamiki TFF bali hucheza tu mechi zao. Kawadanganyeni ' Wapuuzi ' wengine juu ya hii sababu ila siyo Mimi na wala sikubaliani nayo kwa 100% kuwa eti hapa tumehujumiwa ila ninachojua Simba SC tumejihujumu wenyewe Jumamosi iliyopita pale ' Kwa Mkapa / Taifa '. Hata kabla ya CAF kubadili hawa Waamuzi wa Simba SC na TP Mazembe Kifo chetu tena cha idadi Kubwa tu ya Magoli / Mabao bado kilikuwa pale pale na tena sasa baada ya Kulalamika hivi wazi wazi kuna uwezekano Kikaongezeka kwani tayari mpaka hapa tulipofikia tumeshawaharibu Kisaikolojia Wachezaji wetu wa Simba SC.
 
Ndugu weka hoja zako zinazopingana na zangu nimeweka mpaka details zangu kuonyesha ni jinsi gani naufatilia mpira! timu zina haki ya kulalamika haijakatazwa ila wanaopanga waamuzi ndiyo wanamamlaka ya kupanga ama kupangua referee tena bila hata sababu CAF wao wapuuzi wamejiwekea mtego wenyewe eti sababu ya kiufundi😡 hapo tutahitaji ufafanuzi zaidi

Ongozana na Timu ili ukakae nyuma ya Golikipa Aishi Manula uwe unamsaidia tu Kuhesabu ' Vyuma ' ambavyo vitakuwa vinaingia Mkuu. Kama Timu bora kabisa ya Club Africaine wamekula ( wamefungwa ) Magoli Nane ( 8 ) kwa bila / sifuri unadhani Simba SC yetu huko itakuwaje? Tena kama Kipa Aishi Manula ' Mjanja ' kuanzia sasa ajifanya ameumia ili asipangwe na achezeshwe Deogratius Munishi ili nae pia ' azikoge ' za Kutosha kama zile Tano Tano ' alizozikoga ' Manula ili wasichekane au kudharauliana.
 
Mimi napingana na mleta mada. Ushauri wangu. Nibora ukae kimya ili kuweka akiba ya maneno. Tuanze kuongea baada ya mechi ya juma mosi. Mimi naomba niweke nukta ntarudi juma mosi baada ya mechi.
 
Ongozana na Timu ili ukakae nyuma ya Golikipa Aishi Manula uwe unamsaidia tu Kuhesabu ' Vyuma ' ambavyo vitakuwa vinaingia Mkuu. Kama Timu bora kabisa ya Club Africaine wamekula ( wamefungwa ) Magoli Nane ( 8 ) kwa bila / sifuri unadhani Simba SC yetu huko itakuwaje? Tena kama Kipa Aishi Manula ' Mjanja ' kuanzia sasa ajifanya ameumia ili asipangwe na achezeshwe Deogratius Munishi ili nae pia ' azikoge ' za Kutosha kama zile Tano Tano ' alizozikoga ' Manula ili wasichekane au kudharauliana.
Nimegundua wewe si shabiki wa simba wala mwanachama wa simba ila ni mnafiki wa simba.

Huzijui figisu walizofanyiwa club africaine? Wale wanatoka taifa ambalo wanacheza mpira usiku kumetulia nyuzi joto ikiwa 7-12 Congo walichezeshwa saa nane jua kali na kapeti unajua linavyochemka
 
Msijitafutie adhabu tafadhali hao ni CAF sio TFF yenu andaeni ushahidi, unless otherwise
 
Ongozana na Timu ili ukakae nyuma ya Golikipa Aishi Manula uwe unamsaidia tu Kuhesabu ' Vyuma ' ambavyo vitakuwa vinaingia Mkuu. Kama Timu bora kabisa ya Club Africaine wamekula ( wamefungwa ) Magoli Nane ( 8 ) kwa bila / sifuri unadhani Simba SC yetu huko itakuwaje? Tena kama Kipa Aishi Manula ' Mjanja ' kuanzia sasa ajifanya ameumia ili asipangwe na achezeshwe Deogratius Munishi ili nae pia ' azikoge ' za Kutosha kama zile Tano Tano ' alizozikoga ' Manula ili wasichekane au kudharauliana.
Hahahaha nimejikuta nacheka mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipotezi muda na Watu walioanza Kuujua na Kuufuatilia Mpira wa Miguu pale Jose Mourinho alipoibuka na kuwa Kocha wa Chelsea tafadhali. Huna ubavu wa Kujenga Hoja na Mimi hasa katika Medani hii ya Mpira kwani achilia mbali tu Kuuchambua na Kuujua pia nimeucheza sana tu na pengine isingekuwa Ukali wa Wazazi na kutaka nijikite zaidi katika Masomo na kutopenda Mtoto wao niwe Mchezaji enzi hizo kuna uwezekano GENTAMYCINE ningekuwa nimeshamtangulia Mbwana ' Popa ' Samatta Siku nyingi mno huko Ulaya ( Ng'ambo ) Siku ukipata muda uwe unatembelea Viwanja vya Barafu au Garden uwe unaona ninavyofanya vitu vyangu hasa sehemu ya Kiungo au Beki Mbili na Tatu. Karibu sana!
Kwa mikwara kaka haujambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ulofa wake huko wapi mkuu,
nini alichoandika ambacho no uwongo,
shida yetu tunapenda kuambiwa maneno mazuri tu ya kutufurahisha, hivi kwa haya malalamiko ya viongozi wenu uoni kwamba yanawavunja moyo wachezaji, naungana na mleta Uzi hii tabia ya kupenda kusifiwa tuu hats ambapo hatusitahili ikome.
Wewe ni lofa. Kwanini wasilalamike??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha msingi simba wajipange kwa mwakani.
Ukweli humweka mtu huru.
mpira huwa unadunda uwanjani na chochote kinatokea...hao hao tp mazembe last season hatua kama hii walikutana ua timu ya angola..mechi ya kwanza ugenini wakatoa sare bilabila mechi ya pili nyumbani wakatoa sare mojamoja wakatolewa...kwa hiyo waangola wangekuwa na akili kama zako baada ya mechi ya kwanza wangesema wajipange kwa mwakani badala ya kujiandaa vizuri kwa mechi ya pili
 
Back
Top Bottom