Nitakuzaje biashara yangu

Joined
Dec 31, 2018
Posts
15
Reaction score
11
Jamani samahanini, mimi ni mgeni humu JamiiForums. Kwa sasa nipo Bagamoyo nimemaliza Advance mwaka huu lakini chuo nitaenda next year.

Baada ya kurudi jeshi mujibu wa sheria, nimefungua duka langu la nguo but still bado halijawa kubwa. Naombeni msaada nitakuzaje biashara yangu au nitapata wapi nguo bei ya jumla nzuri kwa bei nafuu, kwa maana mtaji wangu bado haujaiuwa Sana.

Asanateni
 
Hizo nguo kwa sasa unachukulia wap?
unauza nguo za grade gani?
unauza nguo za Jinsia gani?

nje ya physical shop unatumia njia gan nyingine kujitanua kibiashara?
Mzigo wa Kwanza nilichukua kariakoo
And ni nguo za kiume
 
Hizo nguo kwa sasa unachukulia wap?
unauza nguo za grade gani?
unauza nguo za Jinsia gani?

nje ya physical shop unatumia njia gan nyingine kujitanua kibiashara?
Natangaza through WhatsApp and also am trying to inform baadhi ya my friends
 
Yan ndo nimefungua kama 3 weeks ago....nimeweka mzigo mara moja tu ambayo iyoo mara moja ilikuw kariakoo
basi lisome soko lako jua wanataka vitu gani,

kuna uzi humu una machimbo ya kariakoo
bila shaka ukifika kule huwa unatafuta bei itakayo kulipa

kuwa na nidhamu na pesa yako,ikiwezekana kwa mwanzoni usiiguse kabisa tumia faida kukuza mtaji

fanya hesabu ya running cost na faida yako kwa umakini

lets say unanunua kadet 17,000
weka usafiri 500
kodi 2000
umeme 100
faida 3000 so itakuwa 22600 kwa kadet moja

faida yako itenge saving 1500
matumizi binafsi 1000
emergency 500

ukifanya hivyo utakuza mtaji...
 
Sawa Sawa nashukur
 
Pia angali wtu wnokuzunguka wantka nini , kama ni T-shirt basi unatafuta chimbo zuri LA T-shirt za bei Nzuri na wewe uuze kwa faida kidogo kulingana na watu wanaokuzunguka ni wa kipato gani ... Pili tangaza bidhaa kwenye social network fb hata insta piga picha safii tangaza ikibidi fanya ads hukosi wateja na biasharaa kukua kwasabb ndo unaanza usiajir mtu piga kazi mwenyew kwanza
All the best
 
Hiyo mind set ya Marafiki ndyo wawe wateja wako achana nayo huwa naikataa kabisa kwenye biashara yeyote utaishia kuwanunia ukiwaona wamevaa nguo mpya ambazo hawajanunua kwako

Kumbuka hizo nguo zinapotengenezwa kule China yule mtengenezaji hakulenga soko lake liwe ni marafiki zake, mwisho hununuliwa na wale asiowafahamu kabisa na ndvyo biashara inataka
 
Asante kwa hii comment. Imenifundisha kitu
 
Enx alot be blessed
 
Ooh sawaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…