NItamjuaje baba wa mtoto!!!

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
5,353
Reaction score
1,234
Wana JF Rafiki yangu mpenzi amekwama, ana huzuni kubwa sana ya yaliyompata. Naomba ushauri wenu. Sitaweza kueleza kila kitu. lakini ni long story.

Kifupi. Ana jamaa ambaye ni mume wa mtu. walianzana naye kama 4 years ago. wakati anamfuata, jamaa alisema kuwa hana mke kwa sasa. Mkewe alifariki. Jamaa alionyesha mapenzi makubwa sana. Baada ya miaka 2, dada akajua kuwa jamaaa ana mke. Kila alilifanya dada ili kumtema jamaa, imeshindikana. Jamaa ni kinganganizi, amejipeleka kwa ndugu wote wa dada eti anadia anataka kuoa. Jamaa habanduki kwa dada, kila siku yupo,. Jamaa ana wivu, dada hana rafiki wala nini! dada hana hata nafasi ya kupata mchumba.

Ikatokea bahari dada amekutana na mtu ambaye wanapanga kuoana, shida atamtemaje jamaa, ambaye yuko violent na anakaba hata corner?
Sasa dada akapanga kuzaa na jamaa ili mimba ikitokea amwambie jamaa ili waachane. Bahati nzuri dada akafanya mapenzi na mchumba siku ya 10 na wakafanya tena siku ya 13 machana. Bahati mbaya siku hiyo hiyo ya 13 jioni jamaa akaja, na dada hakuwa na ujanja wakafanya mapenzi usiku. Dada ikamuuma sana, kwa kuwa hadi sasa hajui baba wa mtoto atakuwa yupo. Mzunguko wake ni 28 days. Msaidieni wana JF, msimcheke, msimchambe, ni ya dunia haya!
 
NA AKOME KUBADILI WANAUME KAMA NGUO, kwani alibakwa au kataka mwnyw? Eti hamtaki jamaa lkn anafanya naye ngono? Huoni unafiki na uuaji, Aende akapime ukimwi ili asije akamwambukiza mtoto,......NB 60% mtoto anaweza akawa wa jamaa mpya
 
NA AKOME KUBADILI WANAUME KAMA NGUO, kwani alibakwa au kataka mwnyw? Eti hamtaki jamaa lkn anafanya naye ngono? Huoni unafiki na uuaji, Aende akapime ukimwi ili asije akamwambukiza mtoto,......NB 60% mtoto anaweza akawa wa jamaa mpya

Angel umekuwa mkali sana! Jamni umeshatendwa! Umewaka moto kama kifuu cha nazi!!! ehh, mwenzako amekwama na anahitaji msaada, wewe unamwakia moto! Haya asante kwa mchano wa mawazo!
 
Kweli dunia tambara bovu! ukalale na wanaume wawili tofauti kwa tofauti ya masaa tu!

Ni kweli kabisa, ila alikuwa hana jinsi! Imagine, kma ni kufikiria kwa mtazamo huo bila kujali case yake, hebu jiulize amelala na wanaume wangapi katika siku 30 zilizopita? Jibu ni 1!!! Swala la masaa, kama liavyoseme, ni bahati mbaya
 
There is always 'jinsi'. Hakupaswa kuwa na uhusiano na watu wawili kwa wakati mmoja. Huyo jamaa mpya anajua uwepo wa wazamani? Anajua kama anataka kuzalishwa ili tu dada ajinasue kwa jamaa yake wa zamani?

Siamini kuwa mtu huwezi kujikwamua kutoka kwa mwanamme kama ukiweka nia thabiti
 



Hapo nakubaliana nawe
 

Hatari sana, wanaume wawili nyama-kwa-nyama siku moja?! Lakini hayatuhusu, hivyo nitastick kwenye kujibu swali lako kadri niwezavyo.

Kusema kweli katika hali hiyo hapo, kuweza kufahamu baba wa mtoto ni mpaka DNA test...au kwa kutumia blood groups (japo hii sio definete lakini inaweza kukupa idea). Kwa kifupi hapo ni mpaka mtoto azaliwe ndio ataweza kujua baba kwa uhakika.

Hii ni kwa sababu....siku ya 10 ni vigumu kupata mimba kama ana mzunguko wa siku 28. Lakini siku ya 13 uwezekano ni mkubwa sana, lakini tatizo alilala kavu na wanaume wote wawili.

Kwa mzunguko wa siku 28, yai kwa kawaida litatoka siku ya 14...hivyo basi, kwa kuwa yeye alilala na wanaume wote siku ya 13 ambapo yai lilikuwa halijatolewa bado, mbegu za wanaume wote wawili zitakuwa zinaranda zikiwa zimechanganyika kwenye fallopian tubes kwa siku nzima zikisubiria siku ya 14 yai litolewe ili zianze kupigania kulirutubisha..na hapo hakuna principle ya 'first in' ndio ana haki ya kurutubisha, kwani mbegu za wanaume wote zitakuwa zinastrugle kutoboa ukuta wa yai la kike ili kuingia na kurutubisha....huwezi kujua mbegu ya mwanaume yupi ilifanikiwa kutoboa na kuingia na kurutubisha!

Asubirie tu DNA au Blood grouping ili kujua baba.
 
NA AKOME KUBADILI WANAUME KAMA NGUO, kwani alibakwa au kataka mwnyw? Eti hamtaki jamaa lkn anafanya naye ngono? Huoni unafiki na uuaji, Aende akapime ukimwi ili asije akamwambukiza mtoto,......NB 60% mtoto anaweza akawa wa jamaa mpya

Angel hiyo 60% imekuja vipi? Sio kweli....hapo ni 50% kwa 50%! Kwani mbegu za wanaume wote zilimwagwa siku ambayo yai lilikuwa halijatolewa bado, na zilifika kwenye fallopiana tube na kusubiri yai litolewe kwa siku nzima...kisha kugombania kurutubisha, na mshindi anaweza kuwa mbegu yeyote toka kwa mwanaume yeyote kati ya hao wawili!
 
Malizia kabisa, bila kinga! UKIMWI kweli haukwepeki!

Mmoja akiwa ni mume wa mtu ambae most probably analala na mkewe kavu pia. Mmoja ni jamaa aliyepatikana hivi karibuni (asiyejua hata uwepo wa mume wa mtu kwenye equation) ambae nae anaweza kuwa analala na mwengine kavu kavu!

Haponi mtu
 
Huyo dada mpumbavu kabisa itakuwa njaa ndo maana inamuuma kumtema huyo mme wa mtu.
 
Mmoja akiwa ni mume wa mtu ambae most probably analala na mkewe kavu pia. Mmoja ni jamaa aliyepatikana hivi karibuni (asiyejua hata uwepo wa mume wa mtu kwenye equation) ambae nae anaweza kuwa analala na mwengine kavu kavu!

Haponi mtu
Mwalimu wangu Gaijin samahani, off topic

Kavukavu unamaanisha nini? Kuna tofauti kati ya kavu na kavukavu?
 
ndugu yng OKADA naomba uniwie radhi km nimekukwaza ila kiukweli NIMEUDHIKA SN kuskia eti MWANAMKE MWENYE AKILI TIMAMU anafanya ngono na wanaume 2 kwa siku 1, huo ni upumbavu na upuuzi, mwanamke unayejiheshimu huwezi kugawa mwili wako hovyohovyo namna hiyo eti kisa jamaa anakung'ang'ania hvy inabidi ubebeshwe mimba na mwingine ili akuache?why? UPUMBAVU HUO tena mwambie akatubu mana amefanya ZINAA, KASEMA UONGO, KATAMANI
 
kweli asilimia 80 ya binadamu ni vichaaa.....
 
Simple,awaite wote wawili wasimame kushoto na kulia kwake. Ateme mate meengi kwenye kiganja cha kushoto,then ayapige na vidole viwili baada ya gumba.yatakaemrukia ndo baba wa mtoto. Kila la kheri
 
mi sina utaalamu wa kidakitari ila tu ushauri wangu akapime na UKIMWI sio mbaya akajua afya yake ili apate kujua aitunze vipi hiyo mimba yake!
 
Mwalimu wangu Gaijin samahani, off topic

Kavukavu unamaanisha nini? Kuna tofauti kati ya kavu na kavukavu?

Jibu la Mchwechwele nafikiri linajitosheleza

hahaha ......loh JF kuna vituko
 
Huyo dada jamani hayuko serious,
atashindwaje kumuacha huyo mume wa mtu kama kweli amedhamiria?

Hapo hana ujanja asubiri tu mtoto azaliwe kama Dr. Riwa alivyoshauri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…