nenda ubungo, kwa wale wauzaji vitabu wanaopanga chini pale nje karibu na vibanda vya kukatia tiketi, mi ndipo nilipotutulia matoleo yote ya Mtobwa like "Tutarudi na roho zetu, najisikia kuua tena, mikononi mwa Nunda, Lazima ufe Joram, Salamu kutoka kusimu, Pesa zako zinanuka, Dar es Salaa usiku, Nyuma ya Pazia na na Zawadi ya Ushindi" Hata hazina iliyolaaniwa cha Eddie Ganzel utakipata pale bila kusahau vya uchumi kama 'the monk who sold his Ferrari, Laws to success and so on'
Dah, nimekumbuka mbali sanaaaa, sijui itapatikana vipi riwaya ile. sikumbuki hata wahusika ila nafaham tu yupo mwanamke mmoja alipata shida sana ndani ya riwaya ile
Mkimbizi nadhani hakijatoka bado,kilichotoka karibuni from the same author ni MDUNGUAJI (The Sniper),ila kama upo Dar waweza muuliza mwandishi/mtunzi wake anaitwa Hussein Tuwa.
Dah umenikumbusha mbali sana,riwaya ya mkimbizi ilifanya ninunue gazeti la kiu,Yule mtunzi Hussein Issa Tuwa anapatikana hata kwenye facebook unaweza kumtafuta.Ukifanikiwa utoe taarifa na sisi tufate