GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
"Watanzania waache kuwekeza sana katika Bajeti za Kunywa Pombe kila mara huku wakishindwa hata tu kukata Bima kitu ambacho nadhani kwa Mtu makini ni muhimu zaidi katika Maisha yake "
Chanzo: Cloudstv 360
Mtani wangu kutoka Mkoani Singida Dk. Mwigulu Nchemba unajua fika kuwa GENTAMYCINE sikukubali kutokana na Uyanga wako, ila nisiwe Mnafiki kwa hiki ulichokisema upo sahihi 100% na nakuunga mkono pia.
Binafsi nitajitahidi sasa nami hizi Bajeti zangu za kununua 'Migoma' ya Kwenu Singida pale Kimboka, Beach Kidimbwi na Maandazi Road Msasani nizielekeze katika Kukata Bima yangu kwani ni Aibu na Upopoma (Upumbavu) kama si Ungumbaru (Ujinga) mkubwa kufanya 'Anasa' huku ukiwa huna Bima yoyote.
Kidogo Mtani wangu Waziri Dk. Mwigulu Nchemba naanza sasa Kuiheshimu hiyo 'Doctorate' yako japo huko nyuma kuna Kauli zako fulani fulani zilikuwa zinanilazimisha nianze Kukupuuza kama si Kukudharau pia.