Mandla Jr.
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 3,098
- 631
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Joseph Selasini ametishia atakuwa wa kwanza kuondoka bungeni kama CCM watafanikisha kampeni zao za kuwashawishi wajumbe wake kutetea misimamo mbalimbali, ukiwamo wa kura ya siri. Alisema kimsingi hakutakuwa na maana ya wajumbe kuendelea na mijadala kama tayari chama hicho tawala chenye wajumbe wengi katika Bunge hilo, kimeshaweka misimamo yake kuhusu mambo kadhaa.
Kama kampeni za CCM kuhusu kura ya siri itapita, mjue hakuna Katiba ya Watanzania. Tutakuwa na Katiba ya CCM. Mimi sitakuwa tayari kutengeneza daraja la CCM la kupitisha mambo yao, nitaondoka kwenye Bunge hili, alisema.
Alisema haoni msingi wa chama hicho kuanza kufanya kampeni kupinga kura ya siri kwa kuwa haitakuwa na masilahi kwake na kwamba huo ni ukiukwaji wa haki ya msingi za raia wa Tanzania katika mchakato wa katiba.
Hata hivyo, wakati Selasini akitoa kauli hiyo, mjumbe mwingine, Juma Nkamia alisema haoni tatizo lolote kwenye kura ya wazi. Kwa mfano mimi natokea Kondoa na mwakilishi wa wananchi wangu, kuna tatizo gani nikipiga kura ya wazi ambayo itawapa fursa wao kujua kama kweli nimefanya walichonituma kufanya, alihoji Nkamia.
Alisema hoja si uwazi au usiri wa kura, bali nia ya dhati ya wawakilishi hao katika kufanya mambo waliyotumwa na wananchi kuja kuwawakilisha bungeni.
Mimi naamini tatizo hapa siyo kura gani, wewe mwakilishi una dhamira kiasi gani ya kuwawakilisha wananchi wako katika mchakato wa Bunge la Katiba.