Nitawezaje kununua Hisa za makampuni yaliyosajiliwa DSE, kama nipo mikoani

ADAM SMITH

Member
Joined
Apr 8, 2014
Posts
81
Reaction score
23
habari wakuu, mimi nipo mkoani na nina mpango wa kununua Hisa sa kampuni mojawapo iliyosajiliwa dse, tafadhari anayejua mchakato wake, anijuze
 
habari wakuu, mimi nipo mkoani na nina mpango wa kununua Hisa sa kampuni mojawapo iliyosajiliwa dse, tafadhari anayejua mchakato wake, anijuze
nenda bank ya crdb,tawi lililo karibu .huwa crdb ni mawakala wa Dar stock exchange
 
Unanunua tu kama vifurushi vya maongezi
 
nenda bank ya crdb,tawi lililo karibu .huwa crdb ni mawakala wa Dar stock exchange
Aisee kama issue huijui sio lazima u comment! Tangu lini CRDB wakawa wakala wa DSE?? CRDB ni moja tu ya makampuni yaliyoorodhesha hiza pale DSE ili ziuzwe! Acha kabisa kumpotosha jamaa.
Ili kununua hisa, ni lazima kununua kutoka kwa wakala. Wakala wanao fanya kazi na DSE nadhani wako saba tu hadi sasa. Baadhi yao ni Tanzania Securities na orbit ambao wako pale posta jengo la IPS froo ya saba!
Lakini jamaa anaweza kwenda moja kwa moja DSE pale atapewa listi nzima ya mawakala na atachagua wakala anaye mtaka ili kununua hisa za Kampuni yoyote ile.
DSE wako posta jengo la GOLDEN TOWEL floo 14!
 
CRDB ni wakala wa baadhi ya kampuni chache zilizo sajiliwa na DSE. Ukitaka kununua hisa kwa uchaguzi wako kutokana na jinsi kampuni inavyo lipa gawio (dividends) vizuri na vigezo vingine vya kibiashara, wasiliana na Stock brokers hata kwa simu. Brokers no kama CORE securities ltd, Solomon stock brokers Ltd, Orbit Securities zipo nyingi Google kupata contacts zao.
 

nashukuru kwa maelezo mazuri mkuu, ntayafanyia kazi
 

ngoja niwatafute hawa stock brokers, asante sana
 

crdb ni wakala wa soko la dse kwa hiyo unaweza kwenda tawi lolote la crdb na utaweza kununua au kuuza hisa ya kampuni yoyote iliyoko pale dse. nasema kama staff wa crdb
 
crdb ni wakala wa soko la dse kwa hiyo unaweza kwenda tawi lolote la crdb na utaweza kununua au kuuza hisa ya kampuni yoyote iliyoko pale dse. nasema kama staff wa crdb

Duh cjawahi kuckia hii kitu ila inawezekana... Sasa mbona dse kwenye website hawajamtaja crdb kama ni mmoja wa brokers
 
CRDB ni wakala wa dse akifanya kazi na Solomon stockbrokers, nenda crdb utapata msaada.
 
CRDB ni wakala wa dse akifanya kazi na Solomon stockbrokers, nenda crdb utapata msaada.

Crdb sio wakala wa dse, nyoosha maelezo kwa kusema crdb wanafanya kazi chini ya solomon stockbroker. Tz tuna mawakala 7 tu mpaka sasa.
 
sasa mkuu the game mbona umeni attack tena? hiyo siyo professional behavior or ethic.kwahiyo ni lazima pia uwe na uelewa mpana sio kumeza tu mkuu. CRDB ni mtoa ushauri pia na sometimes unaweza nenda kwao kupata huduma kama wakala wa DSE.kwani hisa za swala zilikuwa zinauzwa wapi?au watu walikuwa wanapanga foleni DSE?
nilimshauri aende CRDB sababu ndio watu wa haraka wanaoweza kumsaidia na kumpa contact na mawakala tofauti na yeye kuwapata mawakala ambao sometimes wanaweza kutokuwa na matawi mikoani.so mimi sijakurupuka na mawakala wote nawafahamu pamoja na washauri na utendaji kazi wao.
orbit securities(dalali na mshauri,255(22)2111758 .STANDARD CHARTERED BANK(mshauri. 255(22)2122160/2122162 UTT/Unit trust of Tanzania(recommended advisor)255222122501/2137592
 
Nataka kuuza hisa zangu za vodacom, kwa anayehitaji au mwenye kumfahamu anayehitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…