nitawezaje kusoma kozi ya 'aeronautics'(aircraft engineering)?

Dogo safi sana kwa kuwa plans mapema.
Kwanza,nmefurahi sana kwa matokeo yenu ya EZEB kuweza kumkalisha Marian mana alikuwa malkia wa iyo kanda kwa kipindi kiref ila nawakmbsha msibweteke mana hao dada ze2 wameenda kujipanga mbaya.Ntafurahi sana km na NECTA mtamkalisha pia.Ila individual performance sijaipenda sana.Endeleen kukaza...
Back to the topic,mi pia nlikuwa na passion na hii k2 ila sikuwa exposed na namna ya kuipata kibongo bongo.Bada ya muda kwa utafiti wang nimegundua njia mbili ambazo unaeza fikia malengo yako;
Kwanza,kuna scholarships wizaran toka Algeria ambao sometimes wanaleta Aeronautics.Hapa itakubidi uisome kwa lugha ya kifaransa.Hawa waarab huitoa mara chache ila isipokuwepo pia unaeza apply coz yoyote alaf baada ya mwaka wa lugha usaili utakapofanyika unajarib kuiomba mana wakat mwingne wanaruhusu kubadili coz.Ila ktk hili nikuonye kuwa huwa wanazingua kwa coz za Medicine,Petroleum na Aeronautics kwa madai ni gharama na watu wengi wanazitaka.Alaf itabid uwe umefaulu vzr advance kwa ilo sina shaka nawe ila kwa coz izo huwa wanazngua ukiwa na F ya G.S.ila faida yake kule unaezapga mpk masters ukipenda through the same scholarship scheme.
Pili,kuna agents flan wanaitwa Global edu. Link hawa ni sawa na Dr George yule agent wa vyuo vya abroad anaekuja Kibaha kila mwaka.Faida ya hawa wanakulink na Sumy State University wanaotoa Aeronautics kwa gharama ndogo.Sasa ww mtt wa kiTz usiwaze kuhusu swala za gharama mana wao wana mkataba na Bank of Africa(BOA) wanaotoa mkopo wa masomo kwa wanafunz wanaokuja huku Ukraine.Pia faida nyingne hapa utaisoma kwa English.Pia matokeo huitaji ya O-lvl na leaving ya Advance tu mana mfumo wao ni tofaut kdogo na wa huko bongo.We wagoogle hao Global ujue wako wap watakueleza kila ki2 ukiridhika unaeza pia ingia nao mkataba.
Nways iyo ni experience yang nloipata bada ya kukosa exposure na hili ndo tatizo kubwa la watoto wa special mana wao huwaza kufaulu tu bila kutafta raman baada ya hapo.Hongera sana kwa kuanza kutafta dira mapema ila usikate tamaa pale utakapo shindwa kufikia malengo uende coz zingne tu ilimrad ukiwa umefaulu vzr v2 vng tu vpo vya kusoma.
All the best boy na salam nyingi sana kwa Mwl Urio.


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ntita yeye alienda kuomba mwenyewe. Alikuwa anasaligi hapo ndo akaomba akapewa. Ndo maana nakushauri usikate tamaa
 
Ndugu yangu MCHUNDO nakushukuru sana.We ni kati ya watu muhimu sana ambao wamenisaidia katika maisha yangu pale nilipohitaji msaada.Mungu akubariki.

Nitawafuatilia hao Global Edu Link. na naomba unapopata taarifa nyingine muhimu kuhusu hili usisite kuniwekea humu jamvini.

Mwl. Urio hatufundishi tena, amepelekwa kuwa Mkuu wa shule Tumbi Sekondari.

Kuhusu matokeo usijali nitajitahidi na nina imani kwa juhudi na kujituma Mungu atatusaidia.

Ila hapo kwenye 'qualifications' za Ukraine sijapaelewa vizuri naomba uniweke sawa.

Asante na Mungu akubariki sana.
 
Dah...Safi sana kwa Mr Urio...
Kwa swala la Ukraine usitie shaka mana hapa wana2mia tokeo la O-lvl kwa mfumo wao.Kwa yule ambae hakwenda Advance itambidi asome mwk 1 wa Pre-University.
Ila kwa ulieenda advance haupigi Pre-Uni mana Advance ni equivalent kwa Pre-Uni but you will have to prove if you went through by providing leaving certificate.Wao hawaitaji tokeo la advance.To get admission here is an easy process so never worry.Hao global wako almost kila mkoa Tz.We wafatilie hao watakupa details zote.
Pia angalia scholarships from Turkey nmeskia pia wanaoffer Aeronautics lakin sina uhakika search net.
Kwa kijana aliefika Special sina shaka na ufaulu wako wa O-lvl hivyo una direct entry qualifications kwa hapa Ukraine.
Kila la kheri mkuu ktk masomo yako.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
nashukuru ndg yangu.

Lakini pia naomba kuuliza, je hapo Ukraine wanahitaji matokeo ya mitihani kama SAT na mingine kama hiyo?
 
Ntita yeye alienda kuomba mwenyewe. Alikuwa anasaligi hapo ndo akaomba akapewa. Ndo maana nakushauri usikate tamaa

nashukuru ndugu yangu, sikati na sitakata tamaa kwani naamini Mungu yupo nami, hataniacha.
 
Hawaitaji pepa zozote mana jamaa wameshafanya elimu kuwa biashara ndo mana wamepunguza masharti mengi...

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hawaitaji pepa zozote mana jamaa wameshafanya elimu kuwa biashara ndo mana wamepunguza masharti mengi...

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

nashukuru sana ndugu yangu.

nimeshawa-google global edu link, nimechukua no zao za simu ndani ya wiki hii ntawatafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…