Kwa yeyote mwenye taarifa,
Wakuu naomba kuelekezwa nikitaka kuwa agent wa kuuza matrekta huku vijijini (mikoa ya Shinyanga na Simiyu) natakiwa kuanzia wapi? Sasa hivi kuna mwamko wa wakulima kununua matrekta (angalau kwa mkopo). Sasa nikitaka niingie ubia na hawa wauzaji wakubwa wa matrekta na zana zingine za kilimo (ambao wengi wameweka makao ya mijini) naanzia wapi?
Ninayo fahamu, wewe ni kuwafuata hao wanao uza au kutoa mkopo, na kukubaliana nao kama utapelekea customers asilimia ngapi utalipwa, kwa mfano atakae nunuu cash asilimia ngapi yako, na atakae chukua mkopo asilimia ngapi na utalipwa vipi, lazima kuwepo maandishi ya malipo na maandishi ya kumkabidhi mteja wako, kuepuka kuzulumiwa.
Asante kwa ushauri Mkuu!!Ili kuwa wakala lazima uwe unafanya biashara yabidhaa ambayo unataka kuwa wakala. Kwa mfano ungekuwa inabidi uwe mfanyabiashara wa zana za kilimo ili uweze kuwa wakala wa matreka. Inawezekana lakini siyo rahisi ukapewa uwakala wa biashara ambayo huna uzoefu nayo.
Kwa kuanzia sajili kampuni ya uuzaji wa zana za kilimo na uanze kununua na kuuza kwa mtaji wako. Baada ya mud kama unafanya vizuri unaweza kuaminiwa kuwa wakal, ambapo sasa utakuwa unachukua mzigo na kulipa baada ya kuuza.