.......nitayasema tu haya bila haya....

.......nitayasema tu haya bila haya....

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2009
Posts
3,400
Reaction score
320
Nitayasema haya,
Bila kuyaonea haya,
Tuuche umalaya,
Utatupeleka kubaya.

Viwili Mola aliumba,
Kutimiza yake namba,
Mme alipomuumba,
Na mke pia akamuumba.

Ni vipi wewe wataka,
Tena tamaa kuwaka,
Rijali umejiweka,
Eti kila mke wataka.

Mwanamme akaweko,
Kasha mke akaweko,
Mwanaume hakuweko,
Na kisha wake kuweko.

Ni kweli kichwa kimoja,
Hubeba ndoo moja,
Ni vipi kichwa kimoja,
Ndoo zaidi ya moja.

Umalaya hulka chafu,
Utatufanya wafu,
Tuenende kwa hofu,
Tena tusiwe vipofu.
 
thanx kaka kwa shairi!
naomba utunge lingine kukumea juu ya mashoga na wasagaji!
wananikera sana!
ubarikiwe!
 
twambie twambie .....usituwache hata kidogo! :gossip:
 
Mkuu heshima yako, wape watu vidonge vyaaoo. Tumekuwa waroho mnooo, hatupitwi na kitu jamani? aghh!
 
Umalaya nayo kazi, kama dobi na mpishi
Umefanyika toka enzi, kufanya watu waishi
Umesaidia vizazi, tuachilie ubishi
Na umesomesha wengi, hivi sasa ni mabosi.

Ni kweli ninakubali, kimaadili ni sumu,
lakini tuseme kweli, kwa wengi kazi muhimu
Kipato cha kwelikweli, wenye maisha magumu
Serikali ihalalishe, kufanya ajira rasmi
 
Umalaya nayo kazi, kama dobi na mpishi
Umefanyika toka enzi, kufanya watu waishi
Umesaidia vizazi, tuachilie ubishi
Na umesomesha wengi, hivi sasa ni mabosi.

Ni kweli ninakubali, kimaadili ni sumu,
lakini tuseme kweli, kwa wengi kazi muhimu
Kipato cha kwelikweli, wenye maisha magumu
Serikali ihalalishe, kufanya ajira rasmi

Ngambo Ngali mekupata,
Pengine ni kutafuta,
Unatufanya kujuta,
Magonjwa yakifukuta.

Siyo vyote vifaavyo,
kuna vingine ni hovyo,
tena havifai hivyo,
tuvitafute halali.
 
Back
Top Bottom