Nitoeni ushamba leo juu ya kuagiza gari mtandaoni

Nitoeni ushamba leo juu ya kuagiza gari mtandaoni

jannelle

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2020
Posts
824
Reaction score
1,581
Nilipita mtandao fulani nikaona Gari, ila kuna sehemu ikawa inanichanganya sana, mfano Gari nimeona USD 2,020, then kwa chini TOTAL PRICE 4,558. Hili ongezeko ni la kitu gani mara mbili yake. Je ni kodi tayari included or hapo ni kuagiza na kusafirisha tu. Msaada picha mfano👉🏼

Screenshot_20250107-001659.jpg
 
Hio total itakuwa shipping fee kama umeweka port ya Dar. Chagua shipping ya roro ipo cheap ya container ipo hali sana.
 
nilipit mtandao fulani nikaona Gari, ila kunasehemu ikawa inanichanganya sana, mfano Gari nimeona USD 2,020, then kwa chini TOTAL PRICE 4,558. Hili ongezeko ni la kitu gani mara mbili yake. Je ni kodi tayari included or hapo ni kuagiza na kusafirisha tu. Msaada picha mfano👉🏼
Hiyo Total Price inaitwa CIF, Cost, Insurance and Freight. Bei halisi ya gari ni $ 2020, mpaka inafika kwenye bandari ya Dar es Salaam itakuwa $ 4,558, Kwa maana inaongezeka gharama ya Insurance and Freight.
Hapo bado tozo ya bandari na TRA.
 
Mmh, kazi ipo wacha tuone
 
Hiyo uliyoona ni bei ya kununua gari bila bima na kusafirisha.

Chini kuna neno CIF (Cost+Insurance+Freight)likimaanisha gharama ya kununua gari, bima ya usafirishaji na gharama za kusafirisha mpaka Dar es Salaam. Ndio maana hapo utaona gharama imeongezeka. Hizo gharama haziusiani na Port Charges za Bandari,Clearing cost,Shipping line,TBS na Ushuru wa forodha(TRA).

Kwa baadhi ya kampuni utakuwa na chaguo wameweka FOB(Free On Board) hii baada ya kulipa manunuzi ya gari, gari lako litasafirishwa bila kulipiwa kutoka Japan mpaka Tanzania. Gari likifika utalipia Tanzania (Final destination) na kwenye hii ni Risk kidogo maana gari wakati wa safari halitokuwa covered na insurance chochote kitachotokea msafirishaji (shipper) hatohusika.

Pia kwenye magari hii option saiz imepungua baada ya Covid19 meli za magari zimekuwa adimu kupatikana na gari ni nyingi hivyo kampuni nyingi hawakubali FOB wanataka ulipe Freight Charges wakupakilie.
 
nilipit mtandao fulani nikaona Gari, ila kunasehemu ikawa inanichanganya sana, mfano Gari nimeona USD 2,020, then kwa chini TOTAL PRICE 4,558. Hili ongezeko ni la kitu gani mara mbili yake. Je ni kodi tayari included or hapo ni kuagiza na kusafirisha tu. Msaada picha mfano👉🏼
Hiyo $2,020 ni bei ya kununulia gari likiwa lipo kule kule Japan.

Lakini sababu lazima likaguliwe, lisafirishwe na meli labda kuja Tanzania na likatiwe bima ya usafiri huo wa meli ili hata ikitokea bahati mbaya labda meli ikazama njiani basi ulipwe jingine, hapo ndio bei inakuja kua $4,558 mpaka gari linafika salama Bongo.

Hapo bado atakuja Mjomba TRA nae anaweza kuja na gharama za kodi ambazo zinaweza kufikia bei hiyo hiyo ya Gari, au kuzidi vile vile.
 
Back
Top Bottom