Nitoke vipi " Bwana misosi"

Nitoke vipi " Bwana misosi"

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
UKWAJU WA KITAMBO
download (1).jpg


NITOKE VIPI - BWANA MISOSI FT HARD MAD VS NIMECHEZEA BAHATI - MAN X FT DULLY SYKES..
______________________________

studio ya Bongo Records ndiyo nyumba kuu ya upishi huu wenye maisha mazuri katika usikivu imara mpaka leo hii.

Ni wazi miongoni mwa wasanii waliowahi kutamba Afrika ya Mashariki katika muziki wa kizazi kipya ni kosa kutomtaja Bwana Misosi kijana toka Tanga.

Na 'Nitoke Vipi' ni wimbo pia ambao ulibeba album kamili ya Bwana Misosi ambayo rasmi ilitoka mwaka 2004. Ikumbukwe wimbo wa Nitoke vipi ulitoka 2003.

Lakini album hii walishiriki watayarishaji watatu ambao ni Mika Mwamba, P Funk Majani na Master Jay.

Lakini jambo baya zaidi hakuna takwimu kamili za mauzo ya album hii lakini ni miongoni mwa album zilizouza kwa ukubwa katika nchi hii.

Na katika album hii kulikuwemo na nyimbo Takribani 8. Nitoke vipi? Feat Hardmad, Mabinti wa kitanga, Upepo unavuma, Tucheze wote Feat Matonya, Kipusa, Mnauliza nini, Nguvu za giza na Nimesomeka.

Ni producer P funk majani ambaye aliweza kutengeneza beat ambayo iliweza kutumia katika nyimbo mbili ( 2) Tofauti ambazo ni "Nitoke vipi " ya Misosi ft hard mad . Beat ambayo baadaye ilikuja kutumiwa na msanii "Alex Kushaba" a.k.a Man x katika kibao chake matata kilichojulikana kama "Nimechezea bahati" ft Dully sykes..

#funguka.

Unadhani ni msanii yupi Kati ya Man x na Bwana misosi aliweza kutumia vyema Beat hilo kutoka kwa kinywele kimoja (1) P funk majani..
 
Unajua haya masanii ya zamani sijui yamerogwa au ni nini hasa, hivi kilichowafanya washindwe kufungua social media accounts kipindi kile zinaanza ni nini hasa? Mtu kama bwana misosi angepaswa kuwa na followers hata 10million instagram…, sasa hapo utapotea vipi?
 
Mkuu,ungekua unaweka na Audio ingependeza zaidi,
Hilo goma nalikubali sana.
 
Back
Top Bottom