Niulize chochote kuhusu Wilaya ya Sikonge Tabora

Wahangaza ndiyo kabila gani waliokuwa wanafanyakazi kwenye mashamba ya Tumbaku toka zao hilo linangia mkoa wa Tabora miaka ya 70 walikuwa Waha na wanyaturu sasa wewe umeka miezi 3 huwezi kujua
Wengi wanaofanya kazi ni Waha, Wahangaza na Wasukuma na wanawake wa kinyamwezi lakini wanaume ni kupendeza wavivu sana
 
Wasukuma hawana umaskini wa kipato,
Sema ni watu wasiojali sana juu ya makazi bora.
 
Wilaya ya Sikonge imeanzishwa mwaka 2001 tu inakuwaje wilaya Kongwe ?
Acheni kuleta Division 5 zenu, kwenye jukwaa la watu wenye akili timamu
Wilaya ya Sikonge ilianzishwa mwaka 1996.
 
Utatakiwa upande basi au gari Moshi mpaka Tabora kisha utapanda basi la Kitunda na hapo ndiyo kuna njia ya Kiloli mpaka Kipili
So nikifika Kitunda ntapanda bus lingine ama ntachukua boda boda? Na hapo Kipili ndio Ipembe?
 
Ha
Nimezungumzia ktk dhana ya mji... mji wa Sikonge ni mkongwe sana.
Kipindi cha nyuma Sikonge ilikuwa imegawanyika sehemu 2 misheni na madukani na madukani ilikuwa ni sehemu ile ambayo maduka yalikuwa yamezunguka ya waraabu
 
Nimezungumzia ktk dhana ya mji... mji wa Sikonge ni mkongwe sana.
Ni mkongwe kwa sababu ya uwepo wa Mission ya Moravian lakini ulikuwa isolated kwa kukosa muunganiko na makao makuu.

Miji mingi ilikuwa inakua kwa kusuasua sana wayaback lakini kuanzia 2005 to 2015 kulikuwa na ukuaji wa haraka sana wa urban na peri urban areas.

Sasa Sikonge haina kivutio chochote kwa watu zaidi ya kilimo ambayo haiwezi kuwa ideal place kwa sababu ya ubovu wa miundombinu na huduma za jamii
 
Acheni kuleta Division 5 zenu, kwenye jukwaa la watu wenye akili timamu
Wilaya ya Sikonge ilianzishwa mwaka 1996.
Kwani wenye division 5 hawana akili timamu ?

Ulipaswa kuweka facts sawa sawa tu siyo kukimbilia division five kwa watu ambao huwajui .
 
Yeah nimewahi kuwa RAS Tabora way back harakati za kuunda wilaya zinaanza
 
Naomba kufahamu gharama zankupanga nyumba hapo sikonge. Nyumba standard iliyoko ndani ya geti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…