Niulize swali lolote kuhusu Geology na field zote zinazohusuhiana na Jiolojia

Samahani mkuu,ni 0783724242 nilikosea namba.
 
Ukisoma Geology, je ajira znapatikana hapa Tz?
Wenzio tunasoma kitu kwa interest.

Sio kwa kuwaza kuajiriwa.

Usitegemee ukimaliza serikari ikukabidhi mgodi ukachimbe bila juhudi zako binafsi.
 
Kama kuna mtu anapatikana merelani

Naomba ani pm nahitaji msaada wake kidogo.
 
Hivi gases na mafuta kipi kinaanza kuchimbwa.maana naskia sehemu yenye gases ujue mafuta pia yapoooo
 
How far from the earth's surface to the core? Nataka kujua juu ya dunia ni wapi?
 
Hivi gases na mafuta kipi kinaanza kuchimbwa.maana naskia sehemu yenye gases ujue mafuta pia yapoooo
Kitaalam kila palipo na oil kuna gas, ila si kila palipo na gas kuna oil.

Kuchimbwa au kutokuchimbwa inategemea na target ya kampuni husika, kama ni oil au gas au vyote.

Pia, huwa hawachimbi tuu kila wanapokuta 'petroleum' (oil n gas), pia huangalia iwapo reserve iliyopo wanaweza kuchimba kwa faida au lah??
 
Upepo husababishwa na nini? je kwa nini sehemu isiyo na upepo(wakusikika) ukiwa kwenye gari au usafiri mwingine utasikia upepo mwingi? nini chanzo chake? je kinaendana na chanzo cha upepo cha kwanza ulicho eleza na kwa nini?
 
Upepo husababishwa na nini? je kwa nini sehemu isiyo na upepo(wakusikika) ukiwa kwenye gari au usafiri mwingine utasikia upepo mwingi? nini chanzo chake? je kinaendana na chanzo cha upepo cha kwanza ulicho eleza na kwa nini?
Upepo husababishwa na tofauti ya mgandamizo wa hewa, kuttoka kwenye mgandamizo mkubwa kwenda mdogo.

Juu ukiwa ndani ya chombo cha usafiri, naweza kusema ni kwa sababu ya tofauti ya mwendokasi wa chombo cha moto na ya upepo. Hivyo hufanya upepo kusikika kama unavuma kwa sana..
 
Kuna tofauti gani katika "geology" na "petroleum geology"
Petroleum geology ni tawi la geology, ambalo huusika zaidi na shughuli zote za utafutaji na uzalishaji wa mafuta ghafi (petroleum).

Hivyo basi, geology kwa ujumla ni pana, matawi mengine ni kama mining geology (madini) , hyrogeology (maji), n.k.
 
Kama ulikuwa huwezi kujibu kwa kiswahili, kwanini ulimuuliza??
Asante kwa elimu yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…