Niulize swali lolote linalohusu vimelea vya magonjwa na kinga ya mwili

pakamwam

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
516
Reaction score
654
heshima kwenu wote
natoa nafasi ya kuulizwa swali lolote linahusiana na vimelea vya magonjwa, upimaji wake na kinga ya mwili

kama una sehemu unatatizwa na unahitaji kufafanuliwa nitakupa ufafanuzi huo na ushauri wa nini cha kufanya

yapo magonjwa mengi sana, yale yanayoambukizwa na yale yasioambukizwa. yanayoambukizwa mara nyingi husabishwa na vimelea vya magonjwa kama bacteria, fangasi na virus

nitakujibu swali utakalouliza litakaloendana na bacteria, fangasi, virusi, ptotozoa na kinga ya mwili

karibuni
 
Ni vimelea gani wanasababisha kiuvimbe shingoni kisichoisha?
 
Naomba kuuliza hii dawa ambayo wabakwaji huwa wanapewa (nimesahau jina) hiyo dawa nasikia huwakinga na maambukizi ya VVU kama watawahi kuitumia kabla ya masaa 72 nadhani.

Kwanini hivyo virusi vinaweza kudhibitiwa na hiyo dawa ila haviwezi kudhibitiwa kwa mwathirika wa siku nyingi?

Maswali mengine yatakuja.
 
Ni vimelea gani wanasababisha kiuvimbe shingoni kisichoisha?
kauvimbe shingini inaweza kuwa kansa lakini pia unaweza kusababishwa na virus. kwa hapo nenda ukamuone daktari wapime ili wajue ni kansa au ni ktu kingine.wapo virus wanaweza kusababisha kansa lakini kansa nyingi zinatokana na makosa katika mfumo wa chembe zamwili kugawanyika. nenda muhimbili. kipimo hicho kama huna bina ni zaidi ya themanini elfu. pia unaweza kupata huduma hiyo kcmc na bugando na rufaa mbeya
 
hizo dawa tunziita kwa jina la ujumla. zinaitwa post exposure prophylaxis. zinaweza kuzuia virus kusambaa mwilini kwa asimilia sabini hadi semanini kama utaanza kunywa ndani ya masaa sabini na mbili baada ya kubakwa au kutembea na mtu ambaye ameambukizwa
 
Na kwa haya yasiyoambukizwa eg miguu kuwaka moto unajuwa nini ?! [emoji120][emoji102]
sina utaalamu sana huko lakini ushauri wangu, kamuone daktari na uangalie sukari na figo na moyo
 
Kwanini hazina uwezo wa kitibu VVU naomba useme kidogo hapo ili tujue.
 
Kwanini hazina uwezo wa kitibu VVU naomba useme kidogo hapo ili tujue.
kikuweliii bado tiba ya vvu haijapatikana zaidi ya majaribio yanayoendelea.
hizi dawa hazitibu vvu maana hawa vvu wakiingia mwilini wanaingia kwenye chembe na kuwa sehemu ya vinasaba vyako.
ili kutibu na kuondoa vvu kwenye mwili lazima uunde dawa inayoweza kumuua kirusi ndani ya chembe yako ya mwili bila kuiua chembe. hii dawa kwa sasa haipo

dawa zilizopo zinafanya kazi ya kumzuia kirusi asiendelee kuzaliana kwa kuharibu vitu anavyotumia kuzalianazingine huwa zinamzua kuingia kwenye chembe na lakini haziendi kumuua aliyepo tayari kwenye chembe

dawa yoyote ya kuua kirusi utakayotengeneza lazima itaua na chembe za mwili kama cd4 na macrophages ambazo wewe unazihitaji ili kuendelea kuishi

sijui kama nimeeleweka kidogo
 
Naomba nipe ufafanuzi kwa nini magonjwa kama Kipindupindu, Ebola na Mafua ya ndege huzuka kwa msimu, hayapo siku zote kama Maralia.
 

Hizo dawa ni effective kwa kuzuia virusi visikutane na seli ila vikishakutana na seli basi tena hazina kazi yoyote na ndo maana inashauriwa utumie ndani ya masaa 72 muda ambao tunaamini virusi havitakua vimeungana na seli
 
Ooh sawa nimepata majibu mazuri sana na nimejua kazi yake sasa.
Hizo dawa ni effective kwa kuzuia virusi visikutane na seli ila vikishakutana na seli basi tena hazina kazi yoyote na ndo maana inashauriwa utumie ndani ya masaa 72 muda ambao tunaamini virusi havitakua vimeungana na seli
 
Write your reply...Mimi naulizia ugonjwa wa kisukari unawezaje kupunguza kinga ya mwili?
 
Naomba nipe ufafanuzi kwa nini magonjwa kama Kipindupindu, Ebola na Mafua ya ndege huzuka kwa msimu, hayapo siku zote kama Maralia.

Haya huenezwa na hewa kwa hiyo kipindi cha upepo mkali hua yanasambaa kwa kasi na kufika sehemu nyingi ila kipindupindu mara nyingi ni kipindi cha uchafu sana ndio hua kinatokea
 
Asante sana kwa majibu.

Magonjwa gani huwa yanaua kwa mnyororo ukiacha UKIMWI (Yaani kama baba alikufa kwa kifua kikuu basi familia yake huwenda ikawa kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo)
Haya huenezwa na hewa kwa hiyo kipindi cha upepo mkali hua yanasambaa kwa kasi na kufika sehemu nyingi ila kipindupindu mara nyingi ni kipindi cha uchafu sana ndio hua kinatokea
 
Me naomba unisaidie hapa kuna kipnd nilikuwa na mawazo sana nikatokewa na kiuvimbe shingon upande wa kulia ila hakiumi kinauma Mara chache sana hasa nikilala vibaya, swali langu je msongo wa mawazo unaweza kusababisha kutokewa na huu uvimbe shingon maana sahv una kama miez 7 haujaisha bado upo
 
uonapo uvimbe wowote mwilini hasa kama hauna maumivu, hatua ya kwanda nenda kamuone daktari ili upime kansa. ikijulikana kama huo uvimbe sio kansa mathalani ni lipoma hatua nyingine zitaendelea. kitu cha msingi kufanya, nenda haraka ukapima huo uvimbe. nimesema gharama ya kupima na kumwana daktari muhimbili ukienda kama private hizidi laki na kumi yaani 30 kumwona daktari na 80 elfu kupima
 
ebola hinezwi kwa hewa, kipindu pindu huenezwa kwa uchafu. uchafu huu hasambazwa toka mahali pamoja kwena pekinge na inzi. wakati fulani hasa wa mvua huwa inzi wanakuwa wengi na mazingira ya bacteria kustawi kwenye uvyevu na vyakula husababisha uenezaji kuwa rahisi. mafua yanaweza kuenezwa kwa hewa na misimu ya upeop
 
Mkuu mimi nina tatizo la kukosa usingizi
 
samahani
Mkuu mimi nina tatizo la kukosa usingizi
hilo sina utaalamu nalo. mimi niko kwenye vimelea na kinga ya mwili. hilo naomba umwone daktari wa kawaida atakuongoza wa kumwona. unaweza kwa daktari wa kawaida hospitali yoyote ili akuongoze kwa specialist
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…