Niurudiaje ualim jamani?

Tiamaji

Member
Joined
Oct 17, 2011
Posts
33
Reaction score
32
Habari wana JF?,mi ni miongoni mwa walim wa SHORT COURSE. Nilihudhuria mafunzo hayo mwaka 2006 na nikafanya kaz kwa miaka miwili(April 2006- August 2088). Nikaandika barua wizarani kuwa naomba kwenda kusoma lkn mpaka muda wa kureport chuo sikupata barua ya ruhusa hivyo nikalazimika kwenda chuo hvyohvyo..mwaka mmoja baadae yan June 2009 mshahara ulifungwa. Nimeshamaliza masomo yangu ya BBA mwaka huu ninahitaji kurudi kufundisha,je inawezekana kufanya hvyo?,nifuatiliaje suala hilo?. Nashukuru wakuu.
 
Nenda wizarani ukafanye follow up maana file lako la ajira lipo mshahara tu ulikuwa umesimamishwa but ukifanya followup things will be ok
 
Kama alivyosema mdau hapo juu we nenda wizarani maana mwajiri wako wewe alikuwa ni katibu mkuu wa wizara!! Au anzia kwa yule katibu mkuu wa chama cha walimu ni mtu mzuri atakusaidia.
 
jaribu kwenda kwenye ile shule uliyokuwa unafundisha kamwone mkuu wa shule nadhani atakuwa nataarifa za mshahara wako kusimamishwa! kuanzia hapo sasa ndiyo ufuatilie! kama ikishindikana kabisa tafuta tempo shule za kata ni nyingi! wakati unatafuta kazi ya kozi uliyo soma chuo!
 
Leseni mlizopewa zilikuwa na expiry date, si ndio? Pili inaonekana hukuwa na maelewano mazuri na HM wako, otherwise asingeripoti kwamba haupo kituoni Omba ajira upya.
 
asanteni wakuu wote,.kaka Gurta,ni kweli mwishon ckuwa na maelewano na mkuu maana yeye alikuwa hataki mimi niondoke eti kwa kuwa nilikuwa mwl pekee wa mathematics na pia nilikuwa cashier wa shule lkn nililazimika kuondoka baada ya kupata sponsor na alitoa masharti lazima mwaka ule ndo nianze chuo. Jamani sijui nianzie wizarani au chama cha walim,nipo dar kwa sasa nadhani ndo muda wa kujua wapi nianzie.
 
Pole sana ila ucjali utarudi kwenye paylor,siku hizi walimu wote boss wao ni mkurugenzi wa halmashauri nacyo tena wizara wewe nenda shuleni ulikokuwa unafundisha kaangalie taarifa zako then nenda kwa afisa elimu sekondari halmashauri ukiwa na salary slip yako ya april,may na barua yako ya ajira atakusaidia kwenda ofisi ya mishahara kwenda kuangalia kama umefutika au umewekewa STOP PAYMENT .nipigie nitakusaidia kwa maelezo zaidi kwani ninauzoefu na hizo issue 0688118561
 
 
Ina maana umejifukuzisha kazi,vinginevyo ungemend faces na mkuu wako badala ya kusepa.Hata hivyo BBA haitambuliki kama cheti cha ualimu,utaendelea kulamba za dip tu.
 
uku ni kuchanganya mambo, ualimu wa Vodafasta utoke uende kusomea BBA alafu urudi ufundishe!! kwanini ukwenda kusoma B in Edu ili ukawa much competent, ina onekana ualimu uupendi, si-amini kama utakubaliwa kurudi kama utadumu kwenye hiyo fani. so far wenzio wanatafuta mbinu za kukimbia hiyo field ya ualimu we unataka kujitumbukiza au kwa vile huna kazi?
 
ualimu ni kazi kama kazi nyingine usiudharau kwasababu mwalimu ndio aliyekufikisha hapo ulipo
 
Wengi wameongea mambo mazuri, yachukue hayo. Mie nakuongezea kuwa wakati mwingne mshahara unaendelea kuflow na payslip. Ila wajanja wanakula na payslip inatoka. Fuatilia jasho lako. Anza hizo sehemu ulizoambiwa kwa kucheki jina ktk payroll.
 
Ina maana umejifukuzisha kazi,vinginevyo ungemend faces na mkuu wako badala ya kusepa.Hata hivyo BBA haitambuliki kama cheti cha ualimu,utaendelea kulamba za dip tu.

Hata hizo za diploma hawezi kupata sababu hana diploma ya ualimu, aliyokuwa nayo mwanzo ni leseni tu na miaka mi5 ya uhai wa leseni hiyo imekwisha.
Kama kweli anaupenda ualimu, akasome Post Graduate Diploma in Education, akichanganya na hyo BBA yake ndio ataweza kupata tena ajira kamili kama mwalimu.
 
Hapo hakuna kazi tena! Ulikuwa kwenye probation ukaharibu and worse ukaenda kusoma BBA ambayo haitambuliki, hilo halina mjadala jina lako lilifutwa tu simply kwa sababu liliandikwa kwa pencil. By the way wakati huo ulikuwa katika masharti ya temporary terms na sio Pensionable terms. So ni ukweli mchungu inabidi umeze huna kazi hapo na huwezi pata kazi tena ya Ualimu kwa kuwa sasa hivi serikali haiajiri wasiosomea Ualimu. Tafuta tu kazi nyingine Mkuu
 
Hajazarau ila ameongea ukweli, anafikiria mbele zaidi. Kwamba tatizo ni ajira ngumu,

lakini na mimi namshauri afuatilie hiyo opportunity aanze level ya chini kwa head master, afisa elimu wilaya, afisa elimu mkoa mpaka wizarani.

Ubalikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…