Ni kuacha kuiga tamaduni ambazo sio zako. Vaa chochote kinachoendana na utamaduni wa huko ulikoolewa kwa maana kwamba tamaduni zinatofautiana kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mfano utamaduni wa Mwafrika kuhusu mke wa mtu ni tofauti na Amerika, Ulaya, Asia n.k. Tatizo linalotokea na pale mtu wa Bara lingine anapoiga utamaduni wa bara lingine kwa kuvaa bila kuzingatia mazingira anayoenda na aina hiyo ya vazi. Kuvaa kunategemeana na matukio, kama unatoka na mume wako kwenda beach na mko kwenye usafiri wenu, si mbaya ukavaa ile mini ambayo kama ukithubutu kuinama, chakala kinakuwa nje. Lakini kama mnaenda arusini tena kuanzia kanisani vaa kama Mmama, maana huko utakutana na watu wa rika tofauti tofauti.