Niwaombe Watanzania "yeyote anayepita jamii za kimataifa kutuombea njaa" tumuone ni mhaini

Nimekuelewa kiasi ingawa bado nahitaji kufahamu:-
(i). Ni kweli kwamba ktk uchaguzi uliopita walikuwemo wahuni wachache ktk kundi la upinzani? (Viashiria vya uhuni wao ni vipi?

(ii). Nchi marafiki kutupa misaada inaweza kuwa hiari yao - lkn je sababu zinazotajwa kutumiwa kutunyima misaada ni sababu zenye uzito au ni nyepesi i.e wanazungumzia uminywaji wa demokrasia - vipigo - na vifo kwa baadhi ya maeneo; je hizi sababu hazina ukweli na uzito?

Machache tu mkuu
 
........ Chaguzi zetu zina mapungufu tena ya kujitakia kabisa, msimamizi wa uchaguzi anapokataa kufuata miongozo ili kupendelea upande flani........
 

Hili bandiko lote ni ili kutetea umwagaji wa damu na zile kura za kwenye mabeg? Ni kwa kuwa tu sina ushawishi kwa mzungu yoyote mwenye nguvu kwenye vyombo vya maamuzi. Ningekuwa na ushawishi huo, ningetaka vikwazo vianze mara moja. Usihalalishe uhuni kwa kigezo cha nchi. Kwani hao walionajisi uchaguzi ww huwezi kuwapelekea huu ujumbe, kuwa uchu wao wa madaraka ni balaa kwetu wote? Ni hivi, ule haukuwa uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hao wazungu kama inawezekana wachukue hatua haraka sana.
 
Hakuna mwanasiasa mwenye mapenzi na wananchi wala nchi yake. Wanasiasa wapo kwa ajili ya utawala na si vinginevyo. Wanasiasa wapo kwa ajili yao binafsi.

Nakubaliana wewe kwa kuliona hilo. Politicians are after Power and no otherwise.

Basi tukabidhi nchi kwa jeshi kisha tufute mfumo wa vyama vya siasa.
 
Bandiko refuuu kama mnyoo wa tendegu, kifupi unachosema, WATAWALIWA WAKUBALI KUWA WATAWALIWA, waachie watawala wawe watawala.

Basi sawa! Ila hujaacha contact.

Everyday is Saturday............................... 😎
 

Ww ni Mjinga mwenye maandishi ya busara.
 

Ule ushenzi tumeuona kwa macho yetu, usidhani tunaongea haya kwa kubahatisha. Rudi shule ukajifunze propaganda, huu utoto uliiongea hapa mpelekee mkweo.
 
Utawala wa kidikteta lazima uondoshwe.
 
Baba yako kila siku anampiga mamaako bila kosa,nani utatangulia kumwonya?

Kipigo kikizidi nani utamsaidia?

Au siku mama yako akipata wa kumsaidia kumpiga babaako,utakasirika au utafurahi?

Ccm mnaongea ushenzi tu.

Hela ya covid wanayodai wazungu ilitoka kwa cdm na act mpk mwone wanachochea?
 
Mhaini wa kwanza ni jiwe na serikali yake kwa kukwapua 1.5T, ningekuona wa maana kama ungekemea, vinginevyo nakuona punguani waheed
 
Tanzania hatujawahi kupigishwa magoti,Never never
 
Nimecheka kwa nguvu, eti ww sio mwanasiasa lakini utetezi na mifano yako yote ni dhidi ya wapinzani! Mbona kwenye mifano yako yote hutolei mapungufu yoyote ya chama tawala, ili tuone how neutral you are?
 
Tanzania hatujawahi kupigishwa magoti,Never never

Ila tuliwahi kupiga mswaki kwa chumvi, kujipaka mafuta ya kula, kufulia na majani ya mpapai, kutumia pipi kama sukari mbadala. Sasa sijui kama kuna kupigishwa magoti kama kule?
 
Hakuna Cha uhain hapa, Cha msingi sio kulalama na kutoa maneno yenye ukakasi bali tujiulize ,tumefikaje hapa, why haikutokea vipindi vyote vilivyotokea iwe leo, nini kimesababisha ,nini kimetokea, kwanini tuko hapa,haya ndo maswali ilitakiwa jiuliza kabla ya kupost, huwezi kimbilia tatua tatizo bila jua chanzo Cha tatizo,
 
Jamaa umeongea point nzuri sana kama baba yako angewaza kama unavyowaza we we hakika tungekua na furaha kilicho Baki hatupigani kwa marungu tunapigana kwa hisia ndo mama watu wanatamani ufalme huu ufitinike mpaka basi kisiwepo chochote kitakacho salia salama baba yako alisema hataki uwepo upinzani sasa kama MTU kakukataa utajipendekeza! Noooo lkn alisema hanashida na misaada nchi yetu tajiri tutazalisha wenyewe na tutajiuzia wenyewe hatuna shida na watu wengine manake tumejitoshereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…