Elections 2010 Niwaonavyo Mawakala wa Chadema

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Kwa kweli mpaka sasa mawakala wa Chadema wameonesha moyo wa kizalendo wa hali ya juu sana kwa Tanzania. Kwani ni wakala mmoja wa Chadema kule Maswa aliyetoa taarifa ya mtu aliyepiga kura mara mbili kwa kuwa na karatasi za kupigia kura mbili mbili na kuweza kuhukumia miaka mitatu jela.

Huu ni mfano wa kijasiri, mzuri na kuigwa na mawakala wote wa upinzani katika chaguzi zijazo. Na huyu anastaili tuzo maalum ya 'mwanademokrasia wa kweli'. Taarifa inasema "... akiwa katika chumba hicho, wakala wa Chadema, Bundala Begani alimwona na kutoa taarifa kwa polisi PC Mkwawa ambaye alimkamata mtuhumiwa. ..." [Mwananchi 2/10/2010, p. 11]

Binafsi namshukuru sana Bwana Bundala kwa uadilifu wa hali ya juu! Chadema naomba mtoe tuzo kwa huyu wakala, tafadhari. Pia wanaharakati kama TAMWA pia mtoe tuzo kwa huyu wakala.

Kwa hiyo kwa sasa some limeeleweka kwa wapiga kura na mawakala. Uchaguzi ujao some litatolewa kwa wasimamizi wa cuhaguzi na watalielewa soma kwani kwa sasa wanapewa 'course outline/ syllabus' kwa njia ya people's power!
 
Ningependa Hakimu na mwendesha mashtaka wa kesi hiyo wahamishiwe kisutu.
 
Ni kweli ni vema kumpongeza huyu wakala kwa moyo aliouonyesha. Lakini pia ni vema kuwapongeza mawakala wa vyama vya upinzani kwa kazi wanazozifanya kwani bila moyo wao wa upendo sidhani kama tungeambulia hata kura moja kwani sisiyemu wanambinu nyingi sana za kuiba kura. Hongereni sana.
 
Hilo ni changa la macho, baada ya miezi miwili atapata Msamaha wa Raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…