Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Na Elius Ndabila
0768239284
Baada ya Mh Rais kuwateua Mawaziri wawili, yaani Waziri wa Mambo ya nje Prof Kabudi na Waziri wa Fedha Prof Mpango kumezuka watu wanaoandika mtandaoni kuwa Rais amevunja katiba ambayo inasema Rais atateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri kwa kushauriana na Waziri mkuu.
Wanaojenga hoja hii, wanasema Mh Rais ameteua Mawaziri akiwa bado hana Waziri mkuu kwa kuwa Waziri Mkuu aliyeteuliwa hajaapishwa.
Ni kweli ukisoma Ibara ya 55 ya Katiba ya JMT kifungu kidogo cha kwanza kinasema "Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa mjibu wa Ibara ya 54 ya watateuliwa na Rais baada ya kushauriana na Waziri mkuu". Ibara hii inazungumzia pia upatikanaji wa Manaibu Waziri.
Ibara ya 51(1) ya Katiba ya JMT ndiyo inayozungumza kuwa kutakuwa na Waziri Mkuu atakayeteuliwa na Rais na inasema kabla ya kushika madaraka ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kitakachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
Lakini Ibara hiyo hiyo ya 51(2) inasema kuwa. Waziri mkuu huyo hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge waliowengi.
Hivyo wanaodhani Rais amekosea ninadhani Ibara hii ya 51(2) imetoa majibu kuwa pamoja na uapisho utakaofanywa wa Waziri Mkuu, lakini tiyari kile kitendo cha Bunge kumthibitisha na kupewa kiti maalumu cha kukalia basi majukumu yake ya Waziri Mkuu yalikuwa yanaanza pale. Kwa mkutadha huo, uteuzi wa Mawaziri uliofanyika leo haujavunja katiba kwa kuwa tiyari toka jana nchi ilikuwa na Waziri mkuu baada ya bunge kumthibitisha.
Mwisho katiba Ibara ya 37(1) inampa nguvu zaidi Mh Rais nguvu wakati mwingine kutimiza majukumu yake bila kulazimika kuomba au kushauriwa na mtu yeyote isipokuwa atakapotakiwa na katiba hii au.
Ninadhani sasa mliokuwa mumedhamiria kupotosha, mumeelewa. WAZIRI mkuu yupo tangu pale Bunge lilipomuthibitisha na ndio maana toka jana kiti chake Bungeni hakipo wazi.