Niwasaidieje hawa wanafunzi wa kike?

KEFODAW

Member
Joined
Jul 14, 2013
Posts
34
Reaction score
2
Msaada unahitajika wa jinsi ya kumwokoa huyu mwl wa taaluma mwenye tabia ya kuwataka kimapenzi wanafunzi wa kike ktk sekondari hii. Nikiwa mwl wa nidhamu nilimwita faragha na kumwonya kwa kumweleza madhara na athari ya tabia yake hiyo. Alitulia kidogo tu, hakubadilika bali kabadili tu mbinu. Anajihami kwa kulaumu kuwa watoto wa kike hawana nidhamu/heshima. Huwatongoza na wanapokataa yeye huwachapa viboko na kuwatishia adhabu mbalimbali. Je ungekuwa ktk nafasi yangu na una nia ya kuwaokoa wanafunzi hawa bila kumwangamiza mwalimu wewe ungefanya nini?
 
Mkuu siku hizi kuna vitu vya "kichina" kibao,tumeona polisi feki,traffic feki,wajeshi feki,dokta feki nk:jaribuni kumchunguza huyo ticha labda nae ni ticha wa kichina...
 

aisee inasikitisha sana, yaani mialimu mingine inatia hasira, sijui ina roho ganiii!! yaani haina ata utu!! TABIA MBOVU KABISAAAA!!
 

Wasalaam mkuu kwa ninavyofahamu aliepewa kazi ya kusimamia utendaji kazi wa walimu mashuleni ni wakuu wa shule. Hivyo kutokuwajibika kwa namna yoyoye kunakofanywa na walimu vituo vya kazi kunaripotiwa kwao wao na kwa ninavyoelewa hues wanawapa walimu charge sheet kama pindi wanapofanya makosa kama hilo na mwalimu husika anapopewa charge sheet tatu basi huyo hupelekwa kwa afisa elimu kata kwa hatua Kali dhidi yake. Sasa kimsingi jitu lililolaaniwa kama hilo liticha ni la kuripoti kwa mkuu wa shule haraka kabla halijaleta madhara kama kweli umelionya halikukusikiliza. Ni laana kubwa kwa jitu zima kama hilo kutongoza wanafunzi.Naomba usilete urafiki katika hili ni lazima aadhibiwe, shame on him idiot!
 

kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…