Nazjaz
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 7,730
- 9,088
Leo tarehe 28.10.2020 Airtel kwa kupitia huduma yao ya Airtel Money wamenisababishia usumbufu mkubwa sana, fedheha na kudharaulika kwa hali ya juu.
Nilikuwa nimeenda shambani Bagamoyo kupiga kura kwani ndiko nilikojiandikishia. Niliweza kupiga kura yangu vizuri, nikaingia shambani KUENDELEA na wajibu mwingine.
Baada ya kumaliza kazi za shambani nikaanza kujiandaa na safari. Nikaendesha hadi kituo cha mafuta nikawaagiza waniwekee mafuta ya elfu hamsini. Nikawekewa na kupewa risiti. Nilipoangalia pochi ndogo kwenye handbag nikagundua nimeiacha nyumbani.
Nikamuuliza pump attendant kama naweza kulipa kwa Airtel Money, akanijibu ndio, nikaingia kwenye menu ya miamala *150*60#.
Majibu naambiwa network error, mind you tayari mafuta yamo kwenye tank.
Nikajaribu kupiga namba 100 huduma kwa wateja, kimashine kinaongea utopolo usio na msaada, hamna unaweza kuongea na call center kwa msaada zaidi. Basi wahudumu wa kituo cha mafuta wakaniweka pembeni, nimedhalilishwa Sana, nimetukanwa, nimekebehiwa na nimefanyiwa dhihaka za kila aina, nimeitwa kila jina baya.
Bahati nzuri akatokea mtu ananifahamu, akaja kuangalia nimekutwa na Nini, nikampa kisa na mkasa, A to Z. Akanilipia 50k nikaondoka.
Nimeumia Sana, inakuwaje TCRA iruhusu kampuni ya mawasiliano itoe huduma bila ya kuwa na kitengo cha huduma kwa wateja? TCRA imeshindwa kuset quality control za service providers, nadhani TCRA iko na shida kubwa ya udhibiti.
Ndugu wajuzi naomba kujulishwa hatua za kufuata ili niwashitaki wahuni Hawa washike adabu