Niweke Spensa au Shokap gari kwenye gari inayogusa chini sana?

tRNA

Member
Joined
Jan 10, 2023
Posts
88
Reaction score
289
Habari wadau,

Nina gari Vitz New model lakini ipo chini sana, ukipita kwenye tuta kubwa au rough road yenye mabonde mabonde lazima iguse chini. Najua humu kuna wataalam wa haya mambo mimi sio mtaalam kabisa wa magari!

Katika kutafuta ushauri wa hili swala wengine wameniambia niweke spensa ili gari inyanyuke kidogo wengine wanasema niweke shokap zipo za kisasa gari haigusi chini tena.

Naomba ushauri wataalam katika hili.
 
Hakuna haja ya kibadilisha shock-up tafuta rim ya size 16 na uweke tairi ya 205/ 70R/ 16 ..
Pia kama utaongezea spacer ya Inch moja itakuwa poa zaidi
 
Hakuna Mtanzania mwenye Vitz New model. Sema una gari ya zamani
 
Funga spacer inch 1 tu, tatizo kwisha. Dar kila moja ni Tsh. 5000- 7000 hapo Ilala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…