lahaja = dialect.
Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia. Lahaja za lugha moja zatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.
Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi na siyo lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.
Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:
vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)
vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika (k.m. lahaja maarufu)
vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)
vipengele vya eneo (kitarafa)
Mfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingerezana lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.
Tena,
lahaja za Kiswahili hutofautishwa kulingana na maeneo yake kama Kiamu (kisiwani kwa Lamu), Kimvita (mjini kwa Mombasa), Kiunguja (kisiwani kwa Zanzibar, Kingazija (visiwani kwa Komoro) na kadhalika
==
Lahaja za Kiswahili
Kiswahili kimepatikana kwa namna au lahaja mbalimbali.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza azimio lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar. Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.
Kati ya lahaja za Kiswahili ni zifuatazo:
Kiunguja: kisiwani Unguja (Tanzania) - kimekuwa msingi wa Kiswahili cha Kisasa.
Kimrima: eneo la Pangani, Vanga, Dar es Salaam, Rufiji na Mafia kisiwani (Tanzania)
Kimgao: eneo la Kilwa (Tanzania)
Kipemba: kisiwani Pemba (Tanzania)
Kimvita: eneo la "Mvita" au Mombasa (Kenya). Zamani ilikuwa lahaja kubwa ya pili pamoja na Kiunguja.
Kiamu: eneo la Lamu (Kenya)
Kingwana: Kiswahili cha Kongo
Shikomor: Kiswahili cha Komoro
Shimaore: Shikomor cha Mayotte (Mahore)
Shindzuani: Shikomor cha Anjouan (Komoro)
Shingadzija: Shikomor cha Komoro Kuu
Kimwani: Kaskazini ya Msumbiji na visiwa vya Kerimba
Chimwiini: eneo la Barawa, kusini ya Somalia
Sheng: Kiswahili cha mtaani Nairobi (Kenya) chenye maneno mengi ya asili ya Kiingereza, Gikuyu na lugha zingine za Kenya
==
Kurudi kwenye swali la mleta mada WANGU MTENZI
Swali:
Jibu: kuhusu sababu sijui .... ila nachofahamu ni kuwa
Wakati wa ukoloni wa Uingereza AZIMIO lilitolewa kutumia Kiswahili cha Unguja kuwa Kiswahili rasmi katika Tanganyika, Kenya na Zanzibar
Waingereza walikitumia pia kama lugha ya polisi na jeshi katika Uganda.
.
[/QUO
Ahsante mkuu, nimepata mengi hapa.
swali la nyongeza: Na hii Lahaja ya Kimtangata ni ya maeneo gani hii?
au inaingiliana na Kimvita?