Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Mwenye njaa ni rahisi kurubunika na kusukumwa kufanya lolote ilhali mwenye shibe hupuuzia hata mambo yenye mustakabali wa maisha yake.
Zipo nchi nyingi duniani ambazo zimeingia kwenye historia ya machafuko mabaya kuwahi kuwakumba; kufuatia njaa:-
1. Flour War (Vita ya Unga) ya mwaka 1775 ilichafua Ufaransa.
2. Food Riots (Ghasia za Chakula) za mwaka 1986 ziliitia doa Zambia.
3. Bread Riots (Ghasia za Mkate) za Machi 8, 1917 huko Petrograd (sasa St. Petersburg) ziliihujumu Sovieti.
4. Mwaka 1975 Mwl Nyerere aliagiza mahindi toka kwa adui yake mkubwa (aliyehujumu jitihada za ukombozi Kusini mwa Afrika) Kamuzu Banda. Media za ughaibuni zilipomhoji kulikoni, alijibu kuwa Mtz asiye na njaa aache kula mahindi toka Malawi.
5. Njaa ilikuwa kigezo cha Mengistu Haile Mariam kuchukuwa Ikulu ya Addis. Mwaka 1985 njaa ya kihistoria iliikumba Pembe ya Afrika na kuathiri Ethiopia kufuatia dola za Magharibi kuisusa kutokana na kung'ang'ania kuistawisha itikadi ya Ujamaa katika Pembe ya Afrika enzi hizo za vita baridi.
Mifupa ya njaa inayotembea (Walking Hunger Skeletons) huko Ethiopia zilimtia huruma Mwanamuziki nguli Michael Jackson almaarufu kama Jacko aliyeongoza dunia kwa kujizolea tuzo 100 ikiwemo ya heshima kubwa na ela nyingi ya Grammy Music Award; na kuamua kutunga wimbo wa kuhamasisha huruma ya dunia kuacha mivutano ya kiitikadi na kuipa Addis chakula. Single yake aliyouza nakala takriban 20ml aliipa jina "We Are the World"
Baada ya kuizindua, meza duara za kidiplomasia (Diplomatic Roundtables) zilijadili misaada kwa Addis na baada ya siku chache metric tonnes za chakula ziliingia Ethiopia.
6. Adolf Hitler katika kuandaa vita kuu ya pili ya dunia (WW II) aliahirisha vyama vya ushirika baada ya kuonekana ni mchwa wa hazina za wakulima. Hitler ili apate chakula cha kutosha kulisha wapiganaji na raia, aliamua kuwaratibu wakulima moja kwa moja tokea Ikulu ya Ujerumani ili kukata mirija ya mapapa wa pembejeo, viuatilifu na mbegu bora. Hizo ni kwa uchache tu.
Ili Kamuzu Banda afanikiwe kuwa rais wa maisha, alilazimika kwanza kuhakikisha kuwa Malawi haiagizi chakula toka nje bali inajitosheleza kwa chakula ndani kwa ndani. Ni rahisi kumtawala mwenye shibe.
Zimbabwe ikaiga Malawi na Afrika Kusini na zote 3 kuitwa Maize Belt (Ukanda wa Mahindi).
Napoleon Bonaparte Kamanda wa Kijeshi na Kiongozi wa Kisiasa wa Ufaransa, Jumapili Juni 18, 1815, alishindwa Vita ya Waterloo kwa kukosa chakula cha raia na wapiganaji. Alijipa matumaini ya kushinda vita na kuteka chakula cha adui (badala ya kulima) Duke wa Wellington.
Baba wa taifa Mwl. Nyerere, mara baada ya vita ya Kagera alibakisha wapiganaji kwenye kambi ya Kijeshi ya Kaboya kulima chakula cha nchi ili kukabili njaa iliyoletwa na vita. Mwl alifanikiwa kwa viwango vya juu kwa jeshi kulisha nchi nzima.
Tanzania inaenda kwenye mikutano ya hadhara ya kisiasa ambayo ni kampeni-kivuli ya kuteka wanachama; bila usalama wa kutosha wa chakula kufuatia wizara ya kilimo na wizara za kisekta km ya biashara na mambo ya ndani kuruhusu mataifa ya Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, DR Congo, Burundi nk kusomba chakula (tena ghafi) moja kwa moja toka mashambani na kwenye akiba za wakulima.
Hivi sasa taifa limefikwa na upungufu na kukimbilia kuagiza chakula toka nje kwa fedha nyingi za kigeni ambazo zingetumika kwenye mahitaji mengine tusiyo na uwezo wa kuyazalisha ndani ya nchi.
Kwa upinzani wenye uzoefu, upinzani ambao haujanunuliwa, njaa hii ni agenda tosha ya kuyateka Bunge na Mabaraza ya Madiwani 2025 lakini pia kwa kuanzia sasa kuteka majimbo na kata zitazokuwa wazi kwa ajili ya chaguzi ndogo. Hizi chaguzi ndogo ndizo kipimo cha upinzani kwa ajili ya 2025.
Kwa kutumia agenda ya njaa inawezekana kwa wapinzani kushinda chaguzi zote ndogo zitazofuata kuanzia sasa.
Mwenye masikio na asikie, mwenye macho na aone, asomaye na afahamu.