Njaaaaa,........

Njaaaaa,........

nkowowo

Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
29
Reaction score
3
Ninasikia njaa kila baada ya saa moja, baada ya kumaliza kula chakula, nimekunywa dawa za minyoo haijanisaidia, naombeni mnisaidie maana maisha na bajeti ya sasa hayaendi.
 
Mkuu, chakula kinapowekwa mezani, usifikiri uko peke yako mwenye njaa au ukiona sahani ya ugali imekwisha usifikiri mlaji ulikuwa ni wewe peke yako, pengine huenda ulikula robo tu ya chakula kwenye sahani kikaisha.

Ni vizuri ukajenga tabia ya kuombea chakula kwa sala kabla ya kula, tatizo lako litakwisha na utakuwa unakula chakula chote kwenye sahani peke yako.
 
Ninasikia njaa kila baada ya saa moja, baada ya kumaliza kula chakula, nimekunywa dawa za minyoo haijanisaidia, naombeni mnisaidie maana maisha na bajeti ya sasa hayaendi.

Tatizo lako unakula makapi!kula vyakula vyenye kuupa mwili virutubisho na cyo kujaza tumbo!
 
Ninasikia njaa kila baada ya saa moja, baada ya kumaliza kula chakula, nimekunywa dawa za minyoo haijanisaidia, naombeni mnisaidie maana maisha na bajeti ya sasa hayaendi.
Hakikisha kila nusu saa kabla ya mlo wowote unakunywa maji ya kawaida (siyo ya baridi) vikombe 2 (ml 500), subiri mpaka nusu saa ipite ndipo ule chakula. Bonyeza link ifuatayo ukajifunze namna njaa hutokea mwilini uzito na unene kupita kiasi | maajabu ya maji

mh hii kali! kunywa maji ya kutosha pia weka na ratiba maalum ya kula.
 
Inawezekana una stress? Unaweza kukumbuka hali hii imeanza kukutokea lini na ulikuwa unapitia mambo gani wakati huo?
Angalia uwe na ratiba nzuri ya kula milo 3 kamili kwa siku. Kunywa maji kabla ya kula kama alivyoshauri Fadhy. Wakati mwingine hakikisha unakula matunda ama kunywa maji mengi kabla njaa haijakolea
 
Duh! Kwahiyo kwa masaa 16 unayokuwa macho inabidi upige milo 16. Pole sana,
 
Back
Top Bottom