Aaron Arsenal
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 24,501
- 28,711
.
Manchester City wamefungiwa kutoshiriki Michuano ya UEFA kwa misimu miwili (2020-2022) na faini ya Euro Million 30 hii inatokana na kukiuka masherti ya kanuni ya Financial Fair Play (FFP)
.
Sheria hii ilitambulishwa na UEFA ili kusaidia klabu barani Ulaya kuhakikisha mapato ya klabu yaendane na matumizi, kuanzia kusajili wachezaji na kuwalipa, ili kupunguza tabaka kati ya klabu masikini na tajiri
.
Manchester City walianza kuchunguzwa baada ya taasisi ya kuchunguza taarifa za soka (Football Leaks Organization) walizinasa barua pepe (emails) za City hivyo kuzituma kwa jarida la Ujerumani, Der Spiegel ambao walichapisha taarifa hiyo, November 2018 na hapo UEFA wakaanza kuchunguza
.
Inaaminika ni suala la udhamini wa Ettihad (Sponsorship deals Inflation) kuwa thamani ya mkataba ule hauendani na kiasi halisi kilichowekwa, wamiliki wamefoji kuweka pesa nyingi ili kuifanya City iwe na ubavu sokoni na kuiaminisha UEFA kuwa wapo imara kiuchumi na wanafanya malipo kupitia pato la klabu
.
Kamati ya CFCB (Adjudicatory Chamber of the Club Financial Control Body) chini ya Jose da Cunha Rodrigues, wanadai City hawakuwapa ushirikiano kwenye uchunguzi, hii hukumu ilishatolewa tangu January 22, 2020
.
City walishaanza kujiimarisha kama timu kubwa barani Ulaya, miaka 10 iliopita wamebeba EPL mara nne na nusu fainali moja ya UEFA, walianza kukubalika mbele ya wachezaji wakubwa
.
City watapoteza kiasi cha dollar million 100 kutoshiriki UEFA, lakini hata wakirejea itachukuliwa kama timu ndogo kwakuwa points zake zitapungua (Coefficient Points) itachukuliwa kama Lower seed, mara nyingi itajikuta kwenye kundi la kifo hatua za makundi
.
Bado nawaza kama wachezaji wakubwa wataona bado Ettihad ni sehemu sahihi, David Silva anaondoka, Aguero na Sane mikataba inaisha 2021, lakini hatari ipo kwa Kelvin De Bruyne, Sterling, Bernado Silva, Ederson na Mahrez hawa wana mikataba zaidi ya 2022
.
Kutolewa kwa City kunaleta vita kubwa ya Top 5, kila timu inaitaka hii nafasi na ukitazama msimamo EPL, nafasi ya 5 mpaka 14 wamepishana points 9 tu [emoji16] vita hii
.
Ngoja tusubiri rufaa yao