Nje ya 18- Simba VS Mtibwa Sugar

Nje ya 18- Simba VS Mtibwa Sugar

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Swaumu ni chungu cha pili, Meddie Kagere anaingia kambani mara mbili, kuipeleka Simba nafasi ya pili na kumwacha Prince Dube wa pili kwenye orodha ya ufungaji, MK14 haihitaji nafasi mbili kuwapaka pilipili

Rally Bwalya na football ya Ulaya, pass za kuvunja taya, kwenye miguu yake kuna ladha kama za kinanda cha Tuddy Thomas, kwenye kichwa chake kuna akili kama Profesa Mulamula na diplomasia ya soka, mtazame kwenye halfspaces, Mgodi unatembea

What is Thadeo Lwanga? Is the movement of molecules from the region of high concentration to low concentration, mlipobanana sana ataitoa timu kwa one touch, mlipozidiwa ataitoa timu kwa tackling, muiteni nae ataitika, mtumeni yeye

Nimtume nani? Mtume Shomari Kapombe, nimpe maagizo gani? Mwambie aipe timu pumzi kule pembeni, mwambie tunamweka bila winga asilia upande wake, mwambie atupigie V Pass, mwambie Shomari asante pia kwa disciplined overlapping, Asante tutaendelea kumtuma

Unasemaje Mwalimu wa Hesabu? Sina usemi ila let Clatous Chama equal to X, waambie Wanafunzi tunatumia njia ya Substitution, Fact Out All Mtibwa players na muweke Chama, balance equation na hence shown, Maestro huyu, fundi huyu, Asante kwa mechi nzuri

Unasemaje Mwalimu wa Chemistry? Namwomba Luis Miquissone aje kufundisha Chemical Kinetics and Equilibrium, atupeleke na maabara kwenye practical, anatuchanganya sana ,mara beki mara kiungo na mara fowadi, badiliko hili la Kikemikali, mtu sana N'jomba Nchumari

Nani kasema Mitaa imetulea? Mohamed Hussein Zimbwe JR mitaa imemlea, tackling zake za mtaani kabisa pale Magomeni, control zake mguuni ni kelele za usiniumizie, nikumbushe lini hivi karibuni kuna beki anaweza kunyumbulika vile, kutulia vile na kuzima mpira vile, nikumbusheni

Practice makes Perfect Chikwende, ndio kaingia Chuo cha Soka, huku hatubandiki matokeo ya Mshindi, angalia matokeo kwa simu yako tu, sasa kaanza kujifahamu, kajtafuta kajipata, acha apewe dakika, acha aendelee kuimarika, kuna balaa linakuja hapa, tusubiri tu

Na kama mvua inashuka na wacha ishuke, wacha ipige tuone wapi panapovuja.
 
620891e6e0e09b999f3e486c1229313d.jpg
 
Back
Top Bottom