Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363

Njegere Ni chakula cha kawaida kabisa kwa watanzania wengi.Njegere huweza tumika kama sehem ya kifungua kinywa,kiungo cha supu ,kiungo cha saladi na hata kama sehem ya mlo mkuu .

Kuna Namna nyingi sana ya kupika na kuandaa njegere.Hii ni moja ya namna ya kuandaa njegere kama sehem ya mlo mkuu.
Kwenye pishi hili nimetumia Beef masala kama moja ya kiungo.Ingawa kiungo hiki ni maalum kwa nyama,kinaleta ladha nzuri sana kwenye Njegere.Kumbuka tu,Upishi ni sanaa,ubunifu lazima.Usikariri.
Mahitaji
Njegere ½ kilo
Nyanya 3 kubwa
Swaumu ½ kijiko cha chai
Beef Masala kijiko 1 cha chai
Nyanya ya Kopo vijiko 2 vya chai
Maziwa fresh kikombe 1 ½
Karoti Mbili,kata duara
Mafuta vijiko 4 vya chakula
Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha njegere adi ziive,ziwe laini na Maji yakauke.
2.Katika sufuria unga mafuta na kitunguu adi kitunguu kianze kubadilika rangi(usiache kikawa cha brown) ,Ongeza nyanya,nyanya ya kopo,chumvi,swaumu na beef masala.Kaanga adi nyanya na mafuta zitengene ndani ya sufuria.
3.Ongeza njegere na karoti ,kaanga kwa pamoja adi njegere na nyanya zishikane.Ongeza maziwa,chemsha uku unageuza mara kwa mara ili maziwa yasikatike na yasiungulie chini.Chemsha adi upate uzito unaopenda.Tayari kwa kula.


Kama familia inawatoto wadogo basi ongeza kiasi cha maziwa ili upate mchuzi mwingi.watoto wengi hupenda mchuzi wa njegere na si njegere zenyewe.
UKIAMUA KUPIKA BASI PIKA CHAKULA KI ZURI