Njemba yachapwa vibao na mwanamke ndani ya daladala

Njemba yachapwa vibao na mwanamke ndani ya daladala

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
AIBU kubwa jana ilimpata mwnaume mmoja kwa kuchapwa vibao na mwanamke ambaye hakumfahamu kutokana na shida ya usafiri iliyowakumba wawili hao. MWanaume huyo alipigwa vibao na mwanamke ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake ndani ya daladala baada ya mwanamke huyo kukerwa kwa kukanyagwa na baba huyo.

Kabla ya kuchapwa vibao hivyo na mwanamke huyo ambaye hakumfahamu kabisa, mwanamke huyo katika pilikapilika ya kugombania daladala na kufanikiwa kuingia ndani alijikuta amekosa siti na kuchukua ndoo yake aliyokuwa akitoka nayo katika pilikapilika zake na kuikalia sehemu ambayo abiria wanatakiwa wasimame.

Wakati watu wengine wanaingia ndani ya basi hilo mwanamke huyo alijikuta akikanyagwa miguu na kuwapa tahadhari kuwa watu wasimkanyage.

Basi hilo lilivyoanza safari zake na abiria kuzidi kuongezeka kila liliposimama kwenye kituo, kasheshe ilimkumba mwanaume ambaye aliamrishwa na konda asogee nyuma kuwapa nafasi abiria wengine. Mwanaume huyo katika kurudi nyuma alimkanyaga mwanamke huyo.

Ghafla mama huyo aliinuka na kuchukua uamuzi wa kumnasa kibao mwanaume aliyemkanyaga na kumshambulia kwa maneno kuwa amemuumiza hadi anasikia maumivu.

Inaonekana mwanaume huyo alikuwa mstarabu na hakupewa kipaji cha kuongea alimwambia mama huyo maneno mawili tu ‘kwanini unanipiga? Wakati anamaliza mama huyo aliinua mkono na kumuwasha kibao kingine cha pili

Bila kuamini mwanaume huyo ambaye muonekano wake ulikuwa ni bonge la mwanaume aliyejaaliwa umbile kubwa hakubishana na mama huyo na kubaki kimya huku abiria wengine wakionekana kumshambulia mama huyo kwa maneno kwa kitendo chake ambacho si cha kistaarabu alichomfanyia mwanaume huyo.

Mkasa huo wa aina yake ulitokea jana majira ya saa 12:49, ndani ya basi linalofanya safari zake kati ya Mbagala na Kivukoni.

:becky:
 
Matendo kama haya hayawezi kupongezwa kamwe, huyu mama hana ustaarabu hata kidogo! Inafahamika kabisa kuwa usafiri wa Dar ni wa taabu, kama wewe hutaki kukanyagwa basi tumia usafiri wako.
Unajua haya yote yanasababishwa na Ubeijing unaowalinda wanawake mpaka kuwapelekea kukosa ustaarabu huku wakijiona kuwa kwa kufanya hivyo ndo ujasiri na kupingwa kuonewa!!
Upuuzi mtupu.
 
Matendo kama haya hayawezi kupongezwa kamwe, huyu mama hana ustaarabu hata kidogo! Inafahamika kabisa kuwa usafiri wa Dar ni wa taabu, kama wewe hutaki kukanyagwa basi tumia usafiri wako.
Unajua haya yote yanasababishwa na Ubeijing unaowalinda wanawake mpaka kuwapelekea kukosa ustaarabu huku wakijiona kuwa kwa kufanya hivyo ndo ujasiri na kupingwa kuonewa!!
Upuuzi mtupu.

Usikute hana mume au mumewa ana erectile disfunction..sasa frustration anazileta kwa watu wasiohusika..Bwa ha ha ha..
 
Naifaninisha na ile story ya mjamaika (Author MMwanakijiji)
 
Back
Top Bottom