Njia 5 za kumfanya mtoto apende kula

Njia 5 za kumfanya mtoto apende kula

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Je, ulishawahi kushauliwa kumkaba mtoto wakati anapogoma kula?. Je, mwanao anatabia ya kubagua chakula, mfano, Ugali?. Haya ni baadhi ya mambo yanayowachanganya wazazi wengi hata kushindwa kufanya kazi zao vizuri. Zipo sababu nyingi zinazomfanya mtoto kukataa/ kubagua aina ya vyakula. Miongoni mwa sababu hizo ni;
1. Aina ya mapishi; fanya uchunguzi kabla na baada ya mtoto kukataa aina Fulani ya chakula, baadhi ya wazazi hufikiri aina ya mapishi wanayoipendelea pia hata watoto wao watapenda.
2.Kupoteza hamu ya kula kwasababu either ugonjwa flani unaomnyemelea, ama magonjwa ya kinywa.
3.Ukosefu wa madini ya Zinc mwilini
4. Teething ama kuota meno
5.Minyoo ambayo hupunguza hamu ya kula
6. Excess water (unywaji wa maji mengi) ambayo huufanya mwili kushindwa kuabsorb chakula na kumfanya motto kuhisi ameshiba
7.Juice zenye sukari nyingi, humfanya mtoto kuhisi kushiba muda wote na kupoteza radha ya baadhi ya vyakula kama ugali
Interval ya muda wa kula, hii humfanya mtoto kukosa hamu ya kula
Njia za kupunguza na kutatua tatizo:-
1. Chunguza chanzo cha tatizo
2. Mpe vyakula vitokanazo na mbogamboga kama vile mchicha na majani ya maboga
3. Usafi wakati wa chakula ni mhimu, siyo vizuri kuacha uchafu karibu huku mtoto anakula
4.Kubalisha aina ya vyombo vya kulia chakula, tumia vyombo vinavyomvutia mtoto
5.Kula pamoja, familia ishiriki pamoja na mtoto/watoto


A+Kula.jpg


NB: Ukiona tatizo bado ni kubwa, muone daktari wa maswala ya rishe na tiba.
PAZIA 3 @ ECE TEACHER
 
Kama mwanao hali mpeleke kwenye maulid utaona atakavokomaa baada ya kuona watoto wakiswahili wakikamata mpunga kwa jazba
 
Back
Top Bottom