Njia ambazo unaweza ukatumia kupunguza gharama wakati wa ujenzi

Joined
Aug 4, 2018
Posts
34
Reaction score
20
Hi

Leo tujadili kwa pamoja njia ambazo unaweza ukatumia kupunguza gharama wakati wa ujenzi

1. Kuchagua simple design(avoid complex design) au tuseme chagua ramani nzuri na rahisi haina makorokoro mengi , kwa kufanya hivi utaweza kuepuka makorido ambayo hayana umuhimu sana , zaidi ya kuongeza gharama . Ramani iwe simple lakn light na privacy lazima ziwe kipaumbele

2. Wakati wa kuchimba msingi cyo ukuta zote zinahitaji kuchimbiwa msingi so unaweza kuziepuka(non-load bearing wall) hii itasaidia kupunguza gharama wakati wa kujenga msingi . Usije ukaasume unajua make sure mtaalamu kakuonesha ipi ni ya kuchimba na ipi haina ulazima

3. Kama katika eneo lako mchanga ni nafuu kuliko mawe basi usitumie mawe , then badala yake weka kifusi, weka mchanga mwagia maji shindilia weka DPM , weka nondo zako za mkanda(ground beam) then mwaka zege la jamvi

4. Tumia nondo tatu kwa mkanda (triangle beam) au hata nguzo kwa nyumba za chini hakuna mzigo mkubwa sana ambao ni risk
Hakikisha kila hatua kahakiki mtaalamu lakini

5. Ukiweka vizuri zege za jamvi na kuipa level nzuri hautahitaji kuweka rough floor wakati wa tiles work hii inasaidia kupunguza cost

6. Azima mbao za kuzuia zege(formwork) kama kazi yako ni ndogo . Hii itasaidia sana kupunguza gharama kama una kazi kubwa bora kununua kuepusha hasara ya mda

7. Chagua simple roofing design ambayo ni cheap
Kama hidden roof ambayo unaweza save 50% of roofing cost

8. Chagua mafundi au mtaalamu ambaye hatakupa gharama kubwa lakini mzoefu kwenye kazi

9 . Utumiaji mzuri wa material. Usizidishe material . Kuna mda unanunua material yanazidi na huwezi hata kumuuzia mtu ni hasara

10. In advance tutumie mfumo mzuri wa maji safi na taka ambao ni cheap na arrangement iwe nzuri siyo bomba la kwenda kwenye septic tank linatembea mita 20 siyo vzr

NAOMBA ONGEZENI NYINGINE NYINGI

Wanaohitaji kupata ramani na ujenzi nafuu

Whatsup / call +255624004650
 
Hapo namba 7...ni kwamba umekosa namna ya kufafanua ama?
 
Ungeweka na vipimo vyake,roof ikiwezekana na gharama ili kulinganisha km kweli ni cheap
 
Material ktk uezekaji hiyo roof ni zipi na gharama yake ikoje. Maana nimependa hiyo Ramani. Nipe contacts zako
 
tii sheria bila shuruti.
ila mjadala wa namna kupunguza gharama ya ujenzi wa nyumba “low cost, affordable, low income housing” ni mzuri sana. na una tija!
 
Mkuu kuna ramani ya nyumba muundo huo huo "sitaki bati" lakini kila chumba kiwe na choo chake i mean master zote Tatu sio kama hapo hizo mbili.??''.. Pia na washroom ya ndani kama hapo.. Usijui umenielewa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…