Tanzania ni nchi yenye amani iliyosheheni watu wa rika zote. Kijana wa Tanzania Tuitakayo ni mfano wa kisiwa katikati ya bahari.
Hivi ndivyo ninavyomfananisha kijana mmoja aliye katika jamii inayomtegemea nchini Tanzania. Kijana asiyejua la kufanya ilihali uwezo anao. Je! ataikomboaje jamii yake ikiwa hana mwongozo chanya. Na hapa ndipo wazo la ubunifu likanijia.
Kisiwa ni sehemu ndogo ya ardhi iliyozungukwa na maji ya bahari, licha ya kuwa na ardhi ndogo lakini ni sehemu ambayo inavutia watu wengi na wengine hutamani kuhamishia makazi yao huko. Ardhi ndogo ya kisiwani iliyozungukwa na maji ya bahari yenye mawimbi makubwa na dhoruba haijasababisha kisiwa kuonekana dhaifu ukilinganisha na Bara. Huyo ndie kijana wa Tanzania Tuitakayo, ambaye historia ya maisha yake, umaskini na kutokuajiriwa havimsababishii kuwa tegemezi kwa wazazi wake na Taifa pia, bali anasimama kidete na kuwa imara ili wengine wapate kujifunza kupitia yeye.
Hivyo kuna njia na namna kadhaa ambazo kijana anaweza kutumia kujikwamua kiuchumi bila kutegemea kuajiriwa na serikali ama sekta binafsi, na njia hizo ni Kama zifuatazo,
1. Ujasiriamali, Kuanzisha biashara yako ni moja ya njia bora ya kujikomboa kiuchumi. Biashara ndogo ndogo kama vile kuuza bidhaa mtandaoni, kutoa huduma za usafirishaji, au kuanzisha biashara ya vyakula. Kwa kuwa mjasiriamali, unaweza kuwa na uhuru zaidi, kudhibiti mapato yako, na kuwa na uwezo wa kuunda fursa mpya za kipato.
2. Kujenga Ushirikiano na watu tofauti, Kujenga mahusiano na watu wenye vipawa na uzoefu katika maeneo ambayo kijana anavutiwa nayo kunaweza kusaidia kufungua fursa za kibiashara au ajira. Kwa kushirikiana na watu wenye uzoefu, kijana anaweza kujifunza na kupanua upeo wake wa kazi hivyo kupelekea kuwa na mtazamo kwa maisha ya baadae.
3. Kujiendeleza yeye binafsi, Kujijengea msingi imara wa maadili ya kazi, nidhamu, na ufahamu mzuri wa masoko ni muhimu katika kujitengenezea fursa za kibiashara au ajira. Kijana wa Tanzania Tuitakayo anapaswa kuwa na tabia ya kujifunza, uvumilivu, na lengo la kufanikiwa. Hii itamsaidia yeye binafsi kujichochea hivyo kutambua wajibu wake katika familia na jamii kwa ujumla.
4. Kujihusisha na Shughuli za Mtandao, Mtandao ni rasilimali kubwa ambayo kijana anaweza kutumia kwa faida yake kiuchumi. Kwa kuanzisha blogu, kujenga uwepo katika mitandao ya kijamii, kuuza bidhaa au huduma mbalimbali za mtandaoni kijana anaweza kupata mapato zaidi hivyo Uchumi wa mtanzania kwa Tanzania Tuitakayo kukua.
5. Uwekezaji katika Mali, Kijana mwenye mtaji anaweza kufikiria kuwekeza katika mali isiyohamishika kama vile ardhi, mashamba, nyumba na kuendeleza miradi ya ujenzi. Uwekezaji huu unaweza kuleta faida ya kudumu kupitia kodi au mauzo ya mali itakapopanda thamani.
Kwa kuzingatia haya na kwa kujitahidi kufanya kazi kwa bidii na uaminifu, kijana wa Tanzania Tuitakayo anaweza kujikwamua kiuchumi pasipo kutegemea kuajiriwa na hatimaye kuwa na mafanikio katika maisha yake zaidi ya miaka 25 tunayoitazamia.
Kutokana na watu wengi kutokua na ajira za serikalini ama sekta binafsi, Serikali inaweza kuchukua hatua kadhaa ili kupunguza idadi ya watu wasio na kazi au wasioajiriwa Hata pasipo kuwaajiri moja kwa moja serikalini ama katika sekta za watu binafsi. Baadhi ya njia ambazo serikali inaweza kutumia ni pamoja na,
1. Kupunguza vipingamizi vya kuanzisha Biashara, Serikali inaweza kuchukua hatua za kupunguza urasimu na vikwazo vingine vinavyoweza kuzuia watu kuanzisha biashara zao kama vile kupunguza gharama za kuanzisha na kusimamia biashara mfano kodi za mapango au fremu za biashara, pia kuweka Sheria ambazo zitamlinda na kumsaidia kijana kuweza kujiajiri kwa uhuru bila vipingamizi Hii inaweza kuvutia zaidi watu kujiajiri na kuunda ajira kwa wengine hivyo kuboresha uchumi wa Tanzania Tuitakayo kwa miaka zaidi ya 25 Tunayoitazamia.
2. Kuboresha uwezweshwaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanapomaliza masomo. Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutoa mikopo ya Ada na pesa ya matumizi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Ikiwa uwezweshwaji huu utaboreshwa zaidi utaweza kusaidia kupunguza idadi ya vijana wasioajiriwa mitaani.
Uwezweshwaji huo ni Kama vile utoaji wa pesa ya Mkopo ya mtaji kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya HESLB pale tu wanapomaliza masomo yao ili wanapoingia mtaani wawe na mitaji kutokana na kiwango stahiki kilichowekwa na serikali.
Hii itamsaidia kijana kuweza kuwa na mtaji huru na kuuzalisha vyema kwani kuwekeza mtaji kwa pesa ya Mkopo ya matumizi "Boom" inawawia vigumu kutokana na matumizi kuwa makubwa yanayosababishwa na hali tofauti za kiuchumi za kila familia.
Hivyo basi, mwanafunzi ambaye hatautumia Mkopo wa mtaji kwa lengo sahihi hataweza kuwa na sababu ya kukosa kujiajiri ikiwa alipatiwa Mkopo wa mtaji na serikali. Hii itapelekea vijana kujikita zaidi katika uzalishaji Mali kwa kujiajiri pasipo kusubiri kuajiriwa.
3. Kuhamasisha Ujasiriamali, Kwa kuanzisha mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na wawekezaji kunaweza kusaidia katika kupunguza idadi ya watu wasioajiriwa Tanzania. Serikali inaweza kuboresha utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali kupitia semina na mikutano mbalimbali, kutoa mikopo ya riba ndogo, na ruzuku kwa wajasiriamali ili kuwasaidia kuanzisha na kukuza biashara zao. Hii itachochea zaidi vijana kuweza kujiajiri na kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania Tuitakayo kwa miaka zaidi ya 25 Tunayoitazamia.
4. Kuwekeza katika Teknolojia, Serikali ya Tanzania ikiboresha uwekezahi katika matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali kunaweza kuongeza ufanisi wa uzalishaji na kutoa fursa za ajira katika sekta za kidigitali. Mfano, uboreshwaji wa masomo ya TEHAMA na kompyuta mashuleni. Kwa kufanya hivi Serikali inaweza kusaidia kuendeleza ujuzi wa kidigitali na teknolojia katika jamii na Taifa kwa ujumla.
5. Kuwekeza katika Elimu na Mafunzo, elimu ya nadharia bila vitendo ni sawa na mali bila daftari ambayo hupotea bila habari. Serikali inaweza kuwekeza zaidi katika elimu na mafunzo ya ufundi hasa kwa vitendo ili kuboresha uwezo wa vijana na watu wazima kwa ajili ya Tanzania Tuitakayo miaka 25 ijayo. Hii itasaidia kuandaa wananchi wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira kwa ajili ya Tanzania Tuitakayo kwa miaka zaidi ya 25 Tunayoitazamia.
Kwa kuchukua hatua hizi, kushirikiana na sekta binafsi na raia, serikali inaweza kupunguza idadi ya watu wasioajiriwa na kuweka mazingira wezeshi ya ukuaji wa uchumi na ajira nchini. Hatua hizi zinaweza kusaidia kuongeza fursa za ajira na kuboresha hali ya maisha ya wananchi kwa miaka zaidi ya 25 Tunayoitazamia kwa Tanzania Tuitakayo.
NAIPENDA NCHI YANGU.

Upvote
1