SoC02 Njia bora za kupunguza mauaji yahusishayo wivu wa kimapenzi

SoC02 Njia bora za kupunguza mauaji yahusishayo wivu wa kimapenzi

Stories of Change - 2022 Competition

Hamissi Hamza Jr

Senior Member
Joined
Apr 16, 2020
Posts
103
Reaction score
209
Mauajia yahusishayo wivu wa kimapenzi limekuwa Janga kubwa kwa Jamii na Nchi kwa ujumla,Inasikitisha kuona wivu wa kimapenzi ukiteketeza nguvu kazi ya Taifa Kwa vijana kuwa Wahanga wa Janga hili".

Kwa Pamoja tunaweza Punguza tatizo hili kwa kutumia njia zifuatazo,

BAADHI YA DINI ZISIZORUHUSU TALAKA WALITIZAME UPYA SUALA LA TALAKA,

Imefika wakati wa wao kuruhusu uwepo wa taraka Hasa baada ya suruhu kwa wanandoa kukosekana baina yao, Upendo unapofika kikomo hua namna tena ya kuwarudisha kama Mwanzo,Watu wasio Na Upendo kuishi pamoja ni Hatari.

WAZAZI WASIWABEBESHE WATOTO WAO MIZIGO YA UVUMILIVU,

Ni kawaida kwa wazazi wa wana ndoa kuwapa moyo kuendelea na ndoa iliyo na changamoto za kiutu zisizo vumilika kama vipigo na manyanyaso ya kimwili na kihisia,
Hii ni hatari wazazi waelewe hakuna uvumilivu wa vipigo na manyanyaso kuna uvumilivu wa changamoto zingine na za utafutaji wa maisha na si vipigo ikifikia hatua hii wasiwafukuze watoto wao wanaporejea nyumbani kwa kuwarudisha walikotoka.

SEREKALI IONDOE DHAMANA KWA WAHUSIKA WA UNYANYASAJI WA KINJISIA NA MAUAJI,

Serikali iitizame upya sheria ya kuruhusu dhamana kwa wahusika na ioiondoe Maana huishia kumalizana nje na wahanga kwa kuwalipa au kukimbia,

VIJANA WASIINGIE KWENYE UCHUMBA NA NDOA KWA MANUFAA YAO BINAFSI,

Mwisho na Washauri vijana Wenzangu wasiingie kwenye uchumba na ndoa na mtu usie na malengo naye ya kiupendo Maana Huwa Na Mwisho Mbaya,Pia Kama Mkiona Hakuna Upendo kama ilivyo kuwa Mwanzo Njia Bora na Salama ya kuachana ni kutoa Taraka.

Pigia kura uzi huu kama sehemu ya Harakati za pamoja kupunguza mauaji ya yahusishayo wivu wa kimapenzi yanarudisha maendeleo ya Familia,Jamii na Taifa kwa Ujumla".

FB_IMG_1658901500537.jpg

FB_IMG_1658901741299.jpg
FB_IMG_1658901340498.jpg
FB_IMG_1658867616893.jpg
FB_IMG_1658867851668.jpg
 
Upvote 0
La mwisho(kisaikolojia)

Kabla ya ndoa mwanaume na mwanamke wapimwe akili kujua utimamu wao wa akili na kiwango chao cha kivumilia maumivu, isijekuwa wagonjwa wa akili wanafungishwa ndoa na hatma yake ndio haya muyaonayo, hawachelewi kufanya matukio mabaya.
 
Njia peke ni moja tuu. Hamna kufungisha ndoa wala kupewa cheti cha ndoa kama mwanamke sio bikra basi. Hapo hamtasikia tena mtu kumiminiwa risasi saba.
 
Back
Top Bottom