Njia gani ya kudhibiti uharibikaji wa mayai pindi kuku anapokuwa anaatamia?

Njia gani ya kudhibiti uharibikaji wa mayai pindi kuku anapokuwa anaatamia?

Maverick tz

New Member
Joined
Dec 4, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Napenda kujua namna ambayo mtu anaweza kutumia ili kudhibiti uharibikaji wa mayai pindi kuku anapokuwa anaatamia.

Pia kama kuku anataga mayai mengi kuliko yale anayoweza kuatamia ni mbinu gani unaweza kutumia ili kuhakikisha mayai hayo yanatotolewa?
 
Mkuu fanya hivi.

Angalia umbo la kuku kwa kawaida kuku mkubwa na mwenye manyoya mengi huwa tunampa mayai 15 hadi17 tu.
hivyo kama umbo ni mdogo mkadirie maana sisi hatumuoni.

pia fanya hivi akishalalia hayo mayai siku ya 8-10 zisizidi siku10 ingia na tochi iwe ya simu ama kawaida then chukua yai la kuku tengeneza muduara kwenye mkono wako kisha yai liweke kwa chini ya kiganja chakokwa kulibana kisha limulike.

Ukiona hilo yai lina michirizi ya damu ama giza linalo shake ukitikisa yai basi jua wazi hilo yai lina mbegu za jogoo na litatotolewa bila shida yoyote.Pia ukiona yai ni fresh tu halina kitu kula maana halina mbegu za jogoo.

Ahsante sana
 
Back
Top Bottom