Njia gani zuri ya kutuma vifaa vya kielektroniki kutoka UK?

Small Axe

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Posts
652
Reaction score
464
Wadau habarini ya shughuli tafadhali naomba kujuzwa ni njia gani rahisi na kwa haraka endapo ukanunua bidhaa au ukapewa kwa nchi za ulaya na iweze kukufikia hapa bongo kwa njia rahisi..
Je kwa njia ya posta naweza mtu akanitumia? Ama Ems na je inaweza tumwa je mdagani mpaka ika fika bongo?
 
njia gani rahisi na kwa haraka
Hakuna njia rahisi na haraka, Bali

- Kuna njia rahisi - ila mzigo unachelewa kufika.
- Kuna njia ya haraka - bali gharama za kusafirisha ni kubwa.
au ukapewa kwa nchi za ulaya na iweze kukufikia hapa bongo kwa njia rahisi..
Atumumie huduma za posta katika nchi husika na mzigo utakufikia hapa nchini. Sharti uwe na sanduku lako la posta.
Ama Ems na je inaweza tumwa
Ndio mzigo waweza kutumwa kwa EMS na ukakufikia
mdagani mpaka ika fika bongo?
Muda
- Hutegemea njia iliyotumika.
- Njia ya posta huwa ni ndani ya siku 14 hadi 21
- Njia haraka huwa ni ndani ya siku 7 hadi 10

Karibu
 
Asante sn kwa maelezo yako mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…