Utangulizi
Kama vijana tunakabiliwa na kupambana na changamoto nyingi zikiwemo kukosa ajira na mitaji. Kulingana na utafiti wa REPOA 2021 inakadiriwa kuwa vijana 800000 hadi 1000000 huingia kwenye soko la ajira kila mwaka na 50000 hadi 60000 pekee ndio hufanikiwa kupata ajira wakiwaacha wenzao zaidi ya laki 9 mtaani. Kundi hili linahitaji sana kupata mitaji, elimu na mafunzo ili waweze kuanza safari ya kufikia ndoto zao.
Inafurahisha kutambua kwamba Tanzania tuna chombo kinachoratibu utolewaji mitaji kwa Watanzania lakini bahati mbaya utendaji wake hauakisi moja kwa moja jamii ya Watanzania. Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi lilianzishwa mwaka 2005 ili kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa mujibu wa nguzo ya tatu (Upatikanaji wa mitaji) ya sera ya Taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004,sera ya Taifa ya huduma ndogo za kifedha ya mwaka 2017 (NMP,2017),pamoja na sheria yake ya mwaka 2018 (MPA,2018). Lengo la kuanzisha mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini ni kupanua wigo wa utoaji huduma za kifedha pamoja na huduma nyingine za uwezeshaji ili kuwafanya wananchi washiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao (uwezeshaji.go.tz).
Lakini inasikitisha kuona utendaji wa mifuko hii umedorora, haujulikani na hauakisi mahitaji halisi ya jamii iliyokusudiwa. Watanzania wengi hawana ufahamu wa mifuko hii, wenye ufahamu hawana Imani nayo,wenye imani hawafikiwi na kufanya hali ya vijana kiuchumi kuzidi kuwa mbaya wakati bajeti inatengwa kila mwaka kuwawezesha vijana! Kwa mfano mwaka 2014/2015 zilitengwa zaidi ya bilioni 6 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya vijana zikaishia kutumika bilioni 1.8 kwa kukopesha vikundi vya vijana 309 (parliament.go.tz)
Je, ni vijana wachache hivi wanaohitaji uwezeshaji? Je,vijana nchini wanaufahamu mfuko huu? Je wana vigezo vya kukopeshwa? Elimu kuhusu mfuko huu imetolewa kwa kiwango cha kutosha? Je ufanyaji kazi wake unaendana nao au unawaacha nje?
Mageuzi ya kiutendaji na kimfumo ya mifuko hii yanahitajika ili kuendana na hali halisi ya watanzania na kutatua tatizo la mitaji kwa vijana.
Mapendekezo
✓Serikali iunde kamati maalum kutathimini mwenendo wa mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi nchini. Iangalie ufanisi wa mfuko moja moja na kupendekeza namna bora ya kuongeza ufanisi. Mifuko isiyoleta tija au yenye madhumuni yanayofanana iunganishwe ili kuongeza ufanisi.
✓Kianzishwe kitengo cha elimu kwa jamii kuhusu mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuifikia jamii chini kabisa na kuwasaidia kukidhi vigezo ili wakopesheke.
✓Serikali iunde taasisi itayoratibu na kusimamia michakato yote ya maendeleo ya vijana. Taasisi hii isimamie kila mradi,mkakati au mfumo wowote wa kifedha unaolenga kuleta maendeleo kwa vijana nchini na iundwe na watu wenye wivu wa maendeleo ya vijana ili iwe rahisi kubuni miradi inayoakisi hali halisi ya vijana nchini. Taasisi hii ifanye kazi kama jicho la vijana nchini kwa kufanya tafiti mbalimbali halisi kuhusiana na changamoto zinazowakumba vijana wa maeneo tofauti tofauti nchini ili kugundua namna bora ya kuzitatua na kuibua fursa katikati ya jamii zetu ama nje ya nchi kwa manufaa ya vijana wote nchini.
✓Iundwe bodi ya mikopo ya maendeleo ya vijana nchini. Chini ya uratibu wa taasisi ya maendeleo ya vijana nchini,bodi hii isimamie utolewaji wa mikopo (isiyo na riba) na urejeshwaji wa mikopo kwa vijana nchi nzima. Uundwe mfumo wa malipo na utambuzi kwa njia ya mtandao ambapo kila kijana atajisajili kuwa mwanachama wa bodi ili kuomba na kulipa mkopo wake. Mikopo inawezakuwa vifaa ama fedha zitakazotolewa kulingana na utekelezaji wake kama utakavyokuwa umeainishwa na tume ya ukaguzi na uangalizi wa miradi. Kijana yeyote asiachwe njiani kabla hajatimiza mradi wake bali awe na usaidizi na uangalizi wa karibu toka kwenye taasisi,tume na bodi ya mikopo.
✓Serikali iunde tume ya wataalam ili kupembua na kuchakata mawazo na mipango ya biashara au miradi iliyoanzishwa au inayotazamiwa kuanzishwa na vijana wa kitanzania. Tume hii itapitia na kumshauri kijana mtanzania namna bora ya kuanzisha au kutekeleza wazo la biashara au mradi alio nao kabla hajaanza kuutekeleza au akiwa katika utekelezaji. Hii itaufanya mradi,wazo au biashara kutekelezeka kwa kuhakiki uhalisi wa utimizwaji wa wazo,biashara au mradi wa kijana kabla ufadhili. Tume hii iundwe na vijana na wadau wa maendeleo ya vijana wenye uelewa na changamoto za vijana.
✓Taasisi ya maendeleo ya vijana ijenge vituo vya vijana vya kibiashara maeneo tofauti tofauti nchini ili vitumiwe na vijana kutekeleza miradi na kufanyia biashara zao. Kijana asiwe na kero tena ya wapi afanyie biashara na wala bodi iliyomkopesha isijiulize watampata wapi mteja wao. Maeneo yaliyo karibu na vyuo yasisahaulike kujengwa vituo hivi ili kuwasaidia wanafunzi kujifunza kutekeleza mawazo au miradi yao wakiwa vyuoni bado ili watakapohitimu wawe wamefanikiwa kujitegemea. Pia vijengwe maeneo mengine kulingana na uhitaji. Kwa kufanya hivi serikali haitakimbizana na machinga barabarani.
✓Liundwe jukwaa la vijana mtandaoni ili iwe sehemu sahihi ya kupeana habari,taarifa,fursa wao kwa wao au maelezo ya serikali kuhusu vijana. Hapa iwe ni kijiwe cha vijana kuzungumza au kuambiwa yawahusuyo kwa manufaa ya uchumi wao.
✓Serikali ianzishe benki ya maendeleo ya vijana nchini. Fedha zote kwa ajili ya vijana zipitie hapa na vijana waitumie kuweka akiba ya fedha zao bila makato wala tozo.
Hitimisho
Kila siku vijana wanahimizwa wajiajiri na kujitegemea na ni jambo jema. Ni wakati mwafaka sasa wa kuhusisha vijana moja kwa moja kwenye mipango inayohusu maendeleo yao. Vijana ni nguvukazi ya Taifa kwa 55% sawa na vijana milioni 14.2 ya nguvukazi ya watanzania wote (Rejea hotuba ya bajeti ya waziri mkuu 2022/2023). Hawa ni vijana wanaoongezeka kila kukicha. Kuwainua vijana kiuchumi ni kuinua uchumi wa Taifa, ni kuboresha kesho ya watanzania wote,ni kuwa na jamii yenye uchumi imara,ni kupunguza umasikini kwa watanzania.

Upvote
3