Kwa njia ya maji kuna meli za mizigo za aina mbili Azam sea link na sea star. hizi unaweza safirisha hivi.
Ukawapakia mifugo yako kwenye gari lako then gari likaingia kwenye meli hadi zanzibar ukifika unawasha ndinga yako unaenda fanya delivery sehemu husika au
Ukawaambia jamaa wakapakia mifugo kwenye gari zao then wakagikisha mpaka sehemu husika hizo meli zina siku zake za kwenda sio kila siku. Meli inaondoka saa nne usiku saa 12 asubuhi inakuwa imefika.
Kuhusu nyama unaweza safirisha kwa meli hizi au
kwa zile speed boti ambazo zinachukua saa moja na nusu tu na zinaenda kila siku
Kuna boti za aina mbili Azam kilimanjaro na Zanzibar one/zanzibar two
Choice ni ya kwako bei hazipishani sana.
Muhimu zaid fika ofisini kwao kwenye kampuni hizi zote mbili wakupe maelezo then wewe mwenyewe utaamua.
Ofisi za hizo kampuni zote mbili zipo posta bandarini pale ile bandari ya kwenda zanzibar.
Kuna njia nyingine ya magendo hii utasafirisha nyama kwa jahazi. Majahazi yanapatikana bagamoyo kule fanya ukavizie upate connection.
Wanasafiri mida ya saa tano sita saa 10 wapo Zanzibar wanapakua.
Magendo yana risk nyingi ila ndio sehemu ya kujitajirisha hapo maana utakwepa gharama za usafiri na kodi za hapa na pale
Choice ni yako
All the best kuelekea uchumi wa buluu