Njia ipi ya Mpango wa uzazi ni bora kwa wanandoa?

Tumia condom, sema kazi kuzinunua..[emoji1]
Nawashangaa sana mnaoitaja njia ya Calender kuwa ni salama.Nimekuwa mtaalamu wa kutumia calender lakini ilinifelisha mara tatu,hata sasa Wife amenasa kizembe kwa sababu ya hiyo..**** U Calender.
 
Haya mambo haya ni mzani unaelea mda wowote unabenukia upande wa pili.
Hapa nasubiri second born baada ya njia hiyo ya kitambaa kunichomesha.My first born ndio kwanza next month anatimiza mwaka🤣🤣.Hatari sana itakuwa ngumu kumkwepa mzungu na ma njia yake
 
hahahaha nacheka kama mazuri, njia za asili sio za kuziamini kabisa mimi niliwah kuambiwa wapo waganga wanafunga pia nikajisemea huko ndio kujifunga kizaz kwa njia ya ushirikina njia za kisasa shida ni zile side effects zake, zikikupenda had raha zikikuchukia utajuta shida utakazopata
 
Hiyo ya Njia ya kitambaa, Hiyo ni imani potofu mbaya sana.

Watu waliopo kwenye medical field watakubaliana nami..
As a matter of fact, mtu yeyote tu yule akifanya akichekecha akili vizuri (reasoning) ataona wazi kuwa "Kitambaa Method" ni uzushi wa hali ya juu sana. hii itafanya wadada wapate mimba mfululizo.

Njia ya Kuficha kitambaa chenye damu ya hedhi, njia hiyo haina uhusiano wowote wa kuzuia Follicle Stimulating Hormone (FSH), Liutenizing Hormone, wala hakuondoi Human Chorionic Gonadotropin hormone (hCG) pia hakupunguzi kiasi cha Oestrogen Hormone katika mwili mwa mwanamke.
 
Hakuna hata salama hapo zote hizo ni mbaya. Njia salama kiafya ni kucheza na kalenda na kutokumwagia ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
kutomwagia ndani pia siyo njia salama.

Kabla ya sperms kutoka, huwa kwanza unaanza ule ute ute kwa ajili ya kusafisha njia, Sasa ule ute ute unaweza kuja na Sperms pia hata kabla mwanaume hajafikia mshindo (ejaculation).
Sperms zinazokuwepo kwenye ule ute ute nazo zinaweza kusababisha Ujauzito ikiwa maji maji ya uke ACIDITY ndogo. (yes usishangae hapo maji maji ya uke ya acidity kiasi kinacholinda ile sehemu)

Pia ukimwaga nje, kisha ukarudi ndani ya uke kuendelea na Tendo basi hapo sperms mshindo uliopita nazo zinakuwepo zipo kwenye mrija wa njia ya uume (urethra). Hizo sperms nazo zinaweza kusababisha ujauzito.

My take:

Ukishajua siku za kupevuka yai ni zipi, basi hapo unaweza kutumia njia ya Kalenda vizuri.. Na haitakuangusha kwa 99.3%.

Kuwa mvumilivu na subiri mwanamke avuke ovulation. Kisha hesabu siku NNE mbeleni.

Kwa msaada zaidi nenda Fertility Clinic au Zahanati wakupe maelekezo vizuri, jinsi ya kukadiria kujua siku za Ovulation (kupevuka kwa yai la uzazi la mwanamke)

Mimba kutungwa inategemea na Yai Kupevuka, na yai halipevuki kila siku. Pia yai likishapevuka linachukua siku 3 au 4 linakufa kama halitakutana na manii za mwanaume.
 
Nawashangaa sana mnaoitaja njia ya Calender kuwa ni salama.Nimekuwa mtaalamu wa kutumia calender lakini ilinifelisha mara tatu,hata sasa Wife amenasa kizembe kwa sababu ya hiyo..**** U Calender.
jifunze kwanza ovulation ni nini... Pia jifunze kuwa siku 4 baada ya ovulation hilo yai linakufa...
Ukishajua linakufa, hapo unaweza kufanya timing.

kikichokufelisha ni kwamba umemrukia wife tu baada ya kumaliza hedhi.

Hapo lazma uwezekano wa kufeli uwe mkubwa.

Ukiijua kalenda vizuri, na ukajua mzunguko wa mwanamke wa miezi 4 iliyopita, ambayo itakusaidia ili uweze kukadiria siku za ovulation vizuri.. Hapo njia ya kalenda utaifurahia vizuri tu sana na itakuwa effective kwa 99.4%.

Usiwe na papara kumrukia tu mwanamke akishamaliza hedhi, tulia jifunze Ovulation kwanza.

Pia mwanamke ambaye wiki chache zilizopita ndiyo amemaliza kutumia njia za vidonge, sindano na vijiti, wanawake wa hivyo huwa mfumo wao wa hormone unabadilika badilika.. Hivyo kunakuwa na ugumu katika kupangilia njia ya kalenda. Labda atulie kama miezi kadhaa ili hormones zake zikae sawa baada tu ya kuachana na sindano na vijiti.
 
Njia ya kalenda uniasifia je ukakuta siku hiyo ni ya hatari na askari wako kashapiga gwaride utafanyaje
 
Unajua wanawake wengi hawana elimu ya haya mambo, pia wanaume wengi nai vilaza.

Ili kwenda sawa shule yake ni pana sana.. kuna uongo mwingi sana kwenye calender.
Ila calender ni mdanganyifu sana, hajawahi kuwa mkweli anabadilika kama kinyonga [emoji28], ni heri wale majivu tu dada zetu
 
Njia ya kalenda uniasifia je ukakuta siku hiyo ni ya hatari na askari wako kashapiga gwaride utafanyaje
Hapo ndo tatizo lilipo kwa watu wengi, watu wanashindwa kujicontrol mizuka ikishapanda. Askari akishapiga gwaride basiiiiii MTU anasahau taratibu zote hapo anachowaza tu ni kuingia ndani uwanja wa vita na kurusha makombora.

Kitaalamu, njia ya kalenda ni salama sana kama ukijua mizunguko angalau minne (4) ya mwanamke iliyopita, pia ukijua vizuri Ovulation ni nini..., na je yai linakufa baada ya siku ngapi?.... Je mimi niongeze mbele siku ngapi ili yai liwe limekufa kabisa.

ili kalenda iwe salama basi subiri kwanza Ovulation ipite. na usubiri Siku 5 mbeleni.

ili kalenda iende vizuri basi hakikisha mwanamke hajatumia Njia za Uzazi wa mpango za Vidonge, Sindano au Vijiti kwa zaidi ya Mwaka Mmoja.

Njia za Sindano, Vijiti na Vidonge, hizi huharibu kwa muda mfumo wa hormone za upevushaji yai (Follicle Stimulating Hormone na Liutenizing Hormone). Sababu kutungwa kwa mimba hutegemea hizo hormones ambazo ndizo zinazopevusha na kuliandaa yai la uzazi mwanamke.

Na ili njia ya kalenda ifanye kazi vizuri inatakiwa hormone ziwe zimetulia bila kusumbuliwa kwa Vidonge, Sindano au Vijiti.
 
IUCD .... Utanishukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…